HOSPITALI ya wilaya ya kahama mkoani shinyanga inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitanda pamoja na wodi ya wazazi kutotosheleza mahitaji ya wingi wa akina mama wanaufika kujifungua hali inayopelekea kuwepo kwa msomganmano mkubwa wodini.
Hayo yamebainishwa na mganga mfawidhi wa hospitali ya kahama Joseph Fwoma wakati kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi wilaya ilipotembelea hospitalini hapo kuona wagonjwa pamoja na kutoa misaada mbalimbali ikiwemo sukari na sabuni kwa wagonjwa wote waliolazwa.
Fwoma amesema kina mama wanaokuja kujifungua hospitalini hapo ni wengi ambapo kwa siku hupokea takribani wagonjwa zaidi ya 50 huku vitanda vya kulalia vikiwa ni 29 tu hali inayopelekea baadhi ya wagonjwa kulala wawili kwenye kitanda kimoja na wengine kulala chini.
Kwa upande wake muuguzi na msimamizi mkuu wa wodi ya wazazi Zahara Hassan amesema kuwa katika hospitali hiyo takribani kina mama 600 hadi 700 hujifungua kwa mwezi ambapo kati yao 100 hujifungua kwa njia ya upasuaji kutokana na matatizo mbalimbali ya kiafya ikiwemo wengi wao kutokwa damu wakati wa ujauzito.
Aidha katibu wa chama cha mapinduzi wilaya Alexandrina Katabi amesema kuwa katika kutembelea wagonjwa hao wametoa misaada ya sukari kilo 100 pamoja na katoni nne za sabuni ya kufuria ikiwa ni njia moja wao ya kuwafariji na kuona kuwa hata wao wanaguswa na matatizo waliyonayo
Hata hivyo mwenyekiti wa CCM wilaya ya kahama Mabala mlolwa amesema kuwa zoezi hilo la kutembelea wagonjwa ni moja ua utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi katika kuhakikisha kuwa wananchi wake wanapata huduma stahiki wanazozihitaji.
Kwa upande wake mmoja wa wagonjwa a waliolazwa katika hospitali hiyo Stansraus Daniel amesema kuwa amefarijika sana na zoezi hili na kwamba huduma wanazozipata ni nzuri na madakitari na wauguzi wamekuwa msitari wa mbele ya kuwahudumia .
Post a Comment