![](https://fbcdn-profile-a.akamaihd.net/hprofile-ak-prn2/s32x32/1117428_100005767122698_1068328177_q.jpg)
MAADILI NI NGUZO MHIMU YA UONGOZI.
Kumekwepo na jitihada ama za makusudi, ama za kutokujua, ama za kile kinachoitwa kumsafisha mbowe.
Niweke wazi kwamba sikumkosoa mbowe
kuhusu mambo ya mahusiano anayosemekana kuwa nayo na wabunge wake wa
viti maalumu, bali ni kuhusu KUKIUKA KWAKE MAADILI YA UONGOZI.
1)
Kitendo cha kukatisha ziara ya mbunge wake wa kazi maalumu ili
wakakutane Dubai kwa kazi maalumu badala ya kazi ya nchi aliyotumwa tena
arudi toka marekani mpk Dubai kwa fedha za serikali ni matumizi mabaya
ya fedha za umma na ni ukosefu wa maadili ya uongozi. Angemrudisha kwa
gharama zake yaani kwa fedha zake hapo ingekuwa mambo binafsi. Kufanya
mambo binafsi kwa fedha ya umma haiwezi ikawa jambo binfsi. Hivyo
sikukosoa mapenzi yao bali matumizi ya kodi za masikini kwa mambo
binafsi.
2)
Kumlazimisha Afisa wa bunge abadili tiketi ileile iliyokuwa aende
kwenye shughuli ya bunge sasa ageuze aende kwenye kazi maalumu hili sio
jambo binafsi ni matumizi mabaya ya madaraka. Ni kukosa huruma kwa hali
ya juu kwa watanzania.
3)
Kumlazimisha mbunge wake wa kazi maalumu kuachana na safari ya kikazi
na kuacha nchi ikose mwakilishi kwenye kikao hicho huku tayari akuwa
ameshagharamiwa safari hiyo, huku tayari akiwa ameshaziba fursa hiyo
ambaye mbunge mwingine angeweza kwenda kuliwakilisha taifa halafu mbowe
na mtu wake wakaenda kwenye kipaombele chake cha kuburudika dubai ni
ukosefu wa uzalendo kwa Taifa na ni ukosefu wa maadili ya kiuongozi.
Tumeongea
kwakuwa wametumia fedha za umma, tumesema kwa sababu wameacha kazi ya
umma huku wakiwa wamechukua fedha kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha
Tanzania na tunasema kwakuwa wamewanyima fursa wabunge wengene ambao
wangekwenda kuwakilisha Taifa endapo fursa hiyo hangepewa mtu
elibadilishiwa safari ya ya taifa na kuitwa kwa kazi maalumu.
"Ukipewa
kazi ya nchi lazima ujiheshimu" NITASHANGAA SANA NITAKAPORUDI BUNGE
LIJALO NIKIKUTA MBOWE BADO NI KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI
Post a Comment