Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia
hali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Mhe.
Haroun Ali Suleiman katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimuombea dua Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali
Suleiman, alipokwenda kumjulia hali katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia
hali Waziri Mkuu mstaafu Mzee Cleopa David Msuya katika hospitali ya
Taifa ya Muhimbili.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia
hali Waziri Mkuu mstaafu Mzee Cleopa David Msuya katika hospitali ya
Taifa ya Muhimbili.
Picha na Salmin Said, OMKR
Picha na Salmin Said, OMKR
******
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amefika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kuwajuilia hali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali Suleiman, pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya waliolazwa katika hospitali hiyo.
Viongozi hao wamelazwa katika hospitali hiyo wakisumbuliwa na matatizo ya moyo. Wakizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais, wamesema wanaendelea vizuri na kwamba afya zao zinaendelea kuimarika siku hadi siku, tofauti na walipofikishwa hospitalini hapo.
Post a Comment