HATIMAYE Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama
juzi wa walibadili kiwango cha shilingi
3,000 walichokuwa wakitozwa wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya kabla ya
matibabu hati kufikia kiwango cha shilingi 1,000.
Mabaliko hayo yalikuja katika kikao cha cha makisio
ya bajeti ya Halamashauri hiyo kwa mwaka 2014/2015 ambapo Diwani wa viti
maalumu Aoko Nyangusu alipotaka kujua kwanini wagonjwa wamekuwa wakitozwa kiasi
hicho kikubwa cha fedha.
Nyangusu alisema kuwa kiasi cha shilingi 3,000
wanachotozwa wagonjwa ni kikubwa kwani kuna baadhi ya watu hawana fedha hizo
ambazo hutolewa kabla ya matibabu na kuongeza kuwa lazima kipunguzwe ili kila
mtu aweze kumudu gharama za matibabu katika Hospitali hiyo.
Hata hivyo Diwani huyo Aoko Nyangusu alisema kuwa
mbali na kupunguzwa katika Hospitali ya Wilaya pia alipendekeza pia kiwango cha
shilingi 1,000 kilichokuwa kikitozwa katika vituo vya Afya na Zahanati
kipinguzwe pia hadi kufikia kiwango cha shilingi 500.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa
Kahama Felix Kimaryo alisema kuwa suala hilo limeptishwa katika baraza hilo la
Madiwanik na kuongeza kuwa viwango hivyo vya fedha vitapunguzwa ili kila
mwananchi aweze kumudu gharama hizo.
Pamoja na Mambo mengine Halmashauri hiyo ya Mji wa
Kahama imeweza kupitisha kiwango cha makisio ya bajeti ya Mwaka 2014/2015
ikiwango cha shilingi bilioni 35.09 kwa mwaka huo ikiwa ni ongezeko la asilimia
53.37 tofauti na mwaka 2013 ilipokuwa kiasi cha shilingi bilioni 22.2.
Akisoma makisio katika kikao cha baraza la Madiwani
wa Halmashauri hiyo ya Mji Felix Kimaryo
alisema kuwa katika mapato ya ndani wamekisia kiwango cha shilingi bilioni 2.9
huku changamoto kubwa ikiwa ni kujikita katika kuongeza mapato ya ndani.
Aidha Kimaryo alisema kuwa changamoto nyingine ni
baadhi ya wafanyabiashara wa mji wa Kahama kukwepa kulipa mapato katika
Halmashauri hiyo ikiwa sambamba na kukwepa kujlipa ushuru kama sheria
inavyowaangoza katika katika biashara zao wanazozifanya.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo alisema kuwa mikakati
iliyonayo Halmashauri yake ni pamoja na kuhakikisha kuwa inaboresha
usimamizi wa ukususanyaji wa vyanzo vya mapato ya ndani pamoja na kuhamasisha wafanyabiashara kulipa
ushuru kwa mujibu wa sheria.
Post a Comment