Na
Baraka Kizuguto, AntalyaWACHEZAJI
wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani ambao kwa sasa ni makocha wa timu ya
Taifa ya Azerbeijan Berti Vogts na msaidizi wake Wolfgang jana jioni kabla ya
mazoezi waliibuka katika viwanja vya hotel ya Sueno Beach na kuongea kidogo na
makocha wa Yanga, Hans van der Pluijm na Charles Boniface Mkwasa masuala ya
kiufundi kisha kuagana nao na kuwaacha waendelee na progamu yao ya mazoezi.
Vogts amabaye alikuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Ujerumani kwa miaka nane (1990-1998) na kufanikiwa kushinda kombe la Ulaya mwaka 1996, na kufika hatua ya robo fainali ya kombe la Dunia mwaka 1998 alikuwa ameambatana na kocha wake msaidizi Wolfagang .
Kocha mpya wa Yanga, Pluijm jana ameanza rasmi kazi ya kukinoa kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara katika viwanja vya hoteli ya Sueno Beach Side baada ya jana kuiongoza katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK.
Hans ambaye amejiunga na Yanga wiki hii akichukua nafasi ya Mholanzi mwenzake Ernie Brandts amesema atajitahidi kadri ya uwezo wake pamoja na wachezaji na benchi la ufundi kuona wanaisaidia timu kufika hatua nyingine mbele zaidi.
"Siwezi kufanya jambo lolote peke yangu bali kwa kushirikiana kwa pamoja nitafanikiwa, kwani katika mchezo wa jana (juzi) timu iliweza kucheza soka la kujituma na kushirikiana mwanzo hadi mwisho, kitu ambacho ndio falsafa yangu katika ufundishaji," alisema Hans.
Timu ilifanya mazoezi ya asubuhi jana saa 5 kamili kwa saa za Uturuki mpaka saa 6:30 kabla ya kupumzika na kurejea tena mazoezini jioni saa 11 kamili jioni mpaka saa 12:30 ambapo alikuwa akiwaelekeza wachezaji jinsi gani anapendelea wacheze kwa kufuata mfumo wake.
Akiongea na www.youngafricans.co.tz mara baada ya mazoezi ya leo kocha Hans amesema timu ya Young Africans ina wachezaji wazuri ambao wana uwezo binafsi na bado wana nafasi ya kucheza soka kwa kipindi kirefu hivyo kikubwa wanapaswa kuwa fiti muda wote ili waweze kutimiza majukumu yao.
Yanga itaendela na mazoezi leo asubuhi katika viwanja vya hotel ya Sueno kujiweka sawa kwa mchezo utakaofuata wa kirafiki kabla ya kurejea nchini wiki ijayo tayari kwa mikikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi ya Mabingwa.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa akiwa na Wolfagang |
Mkwasa na bosi wake Van der Pluijm |
Mkwasa akiwa na Vogts kulia |

Post a Comment