THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Mhandisi Paul Mhangilwa Masanja kuwa Kamishna wa Madini nchini.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Obeni Y. Sefue mjini Dar Es
salaam leo, Ijumaa, Januari 17, 2014, imesema kuwa uteuzi huo wa Bwana
Masanja ulianza jana, Januari 16, 2014.
Taarifa hiyo imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Mhandisi Masanja alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
Post a Comment