Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa semina ya siku mbili kwa makatibu wa vyama vya
mpira wa miguu vya mikoa kuhusu maboresho ya timu ya Taifa (Taifa Stars).
Semina
hiyo inafanyika ukumbi wa Singida Motel, mjini Singida kuanzia kesho
(Januari 18 mwaka huu) ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa kwa
washiriki kuhusu maboresho hayo.
TFF
imeandaa mpango wa maboresho kwa Taifa Stars ambapo pamoja na mambo
mengine umepanga kusaka vipaji nchini nzima kwa lengo la kupanua wigo wa
kupata wachezaji wanaoweza kuchezea timu hiyo.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premiu Lager mwaka huu inakabiliwa
na mechi za mchujo za Kombe la Afrika (AFCON) ambalo fainali zake
zitafanyika mwakani nchini Morocco.
Mechi hizo za mchujo zitachezwa kati ya Septemba na Novemba mwaka huu ili kupata timu 16 zitakazofuzu kucheza fainali hizo.
WASOMALI KUCHEZESHA YANGA, WACOMORO
Shrikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Somalia
kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na
Komorozine Sports ya Comoro.
Mechi
hiyo ya kwanza ya raundi ya mchujo itafanyika jijini Dar es Salaam kati
ya Februari 7 na 9 mwaka huu wakati ile ya marudiano itachezwa kisiwani
Comoro kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Mwamuzi
wa kati atakuwa Hassan Mohamed Hagi wakati wasaidizi wake ni Hamza Hagi
Abdi, Bashir Abdi Suleiman na Bashir Olab Arab. Kamishna wa mechi hiyo
atakuwa Eugene Musoke kutoka Uganda.
Timu
ambazo zimeingia moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya Ligi ya
Mabingwa ni Coton Sport ya Cameroon, El Ahly (Misri), TP Mazembe
(Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El Hilal (Sudan), Club Sportif
Sfaxien (Tunisia) na Esperance (Tunisia)
Nayo
mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kati ya Azam ya Tanzania na
Ferroviario Da Beira ya Msumbiji itakayofanyika Dar es Salaam kati ya
Februari 7 na 9 mwaka huu itachezeshwa na waamuzi kutoka Sudan.
Waamuzi
hao ni Mutaz Abdelbasit Khairalla atakayepuliza filimbi, Waleed Ahmed
Ali, Aarif Hasab Elton na El Fatih Wadeed Khaleel. Kamishna wa mechi
hiyo ni Hassan Mohamed Mohamed kutoka Somalia. Mechi ya marudiano
itachezwa Msumbiji kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Timu
zilizotinga moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo ni
Asec Mimosas ya Ivory Coast, Ismailia (Misri), Wadi Degla (Misri),
Djoliba (Mali), MAS (Morocco), Bayelsa United (Nigeria), El Ahly Shandy
(Sudan), E.S.S. (Tunisia), C.A.B. (Tunisia) na Zesco United (Zambia).
WATANZANIA KUCHEZESHA MECHI ZA CL, CC
Watanzania
wanane wameteuliwa kuchezesha mechi mbili za marudiano za raundi ya
awali za Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) na Kombe la Shirikisho (CC)
zitakazochezwa wikiendi ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Waamuzi
hao walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Israel
Mujuni atakayechezesha mechi ya CL kati ya Rayon Sport ya Rwanda na AC
Leopards de Dolisie ya Congo itakayofanyika jijini Kigali.
Mujuni
atasaidiwa na Josephat Bulali, Samwel Mpenzu na Ramadhan Ibada, wakati
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Jean Marie Hicuburundi wa Burundi.
Naye
Waziri Sheha ataongoza jopo lingine kwenye mechi ya CC kati ya FC MK ya
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na El Ahly Atbara ya Sudan. Mechi
hiyo itachezwa jijini Kinshasa.
Sheha atasaidiwa na Ferdinand Chacha, John Kanyenye na Israel Mujuni. Kamishna wa mechi hiyo ni Chayu Kabalamula kutoka Zambia.
SEMINA YA KUPANDISHA MADARAJA WAAMUZI JAN 21
Semina
kwa ajili ya kupandisha madaraja waamuzi itafanyika Januari 21 na 22
mwaka huu katika vituo vitatu vya Dodoma, Mwanza na Songea.
Waamuzi
watakaoshiriki katika semina hizo ambazo pia zitahusisha mitihani ya
utimamu wa mwili (physical fitness test) watajigharamia wenyewe na
wanatakiwa kufika vituoni siku moja kabla. Waamuzi hao ni wa daraja la
pili na tatu.
Kituo
cha Dodoma kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam,
Dodoma, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Pwani, Singida na Tanga.
Wakufunzi katika kituo hicho ni Paschal Chiganga, Said Nassoro na Soud
Abdi.
Wakufunzi
wa kituo cha Mwanza kwa ajili ya waamuzi wa mikoa ya Geita, Kagera,
Katavi, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Tabora ni Alfred Kishongole,
Kanali Issarow Chacha, Saloum Chama na Zahra Mohamed.
Kituo
cha Songea ni kwa ajili ya waamuzi kutoka Iringa, Lindi, Mbeya, Mtwara,
Njombe, Rukwa na Ruvuma. Wakufunzi katika kituo hicho ni Charles
Ndagala, Joseph Mapunda, Riziki Majala na Victor Mwandike.
Waamuzi
wote wanatakiwa kwenda katika kituo walichapangiwa. Vilevile wanatakiwa
kuwa na barua kutoka kwa makatibu wa Vyama vya Waamuzi wa Mpira wa
Miguu Tanzania (FRAT) wa mikoa yao ikiwatambulisha pamoja na kuonesha
madaraja yao.
Post a Comment