Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkagua na kumpa pole Waziri wa Kazi
na Utumishi wa Umma Zanzibar Mh. Haoun Ali Suleiman aliye;lazwa katika
Hospitali ya Rufaa kitengo ya MOI Muhimbili Jijini Dar es salaam.Waziri Haroun amelazwa Hospitalini hapo karibu wiki moja sasa akikabiliwa na tatizo la ugonjwa wa Moyo { Blood Pressure }.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR.
Na Othman Ame OMPR
wa Kazi na Utumishi wa Umma wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Haroun Ali Suleiman aliyelazwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Kitengo cha mifupa { MOI } Mjini Dar es
salaam kutokana na matatizo ya ugonjwa wa Moyo{Blood
Pressure}Kesho Jumamosi Tarehe18 Januari 2014 anasafirishwa kupelekwa
Nchini Afrika ya Kusini kwa uchunguzi na Matibabu zaidi ya afya yake.
Hatua za mwisho za safari yake
inayogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimekamilika baada
ya kurejea kwa unafuu wa afya yake iliyokuwa imetengemaa kwa takriban
wiki moja sasa.
Waziri Haroun alipata matatizo ya maradhi
ya moyo Ijumaa iliyopita na kupatiwa huduma za afya Zanzibar na
kutokana na hali yake kutokuwa ya kuridhisha ikilazimika kusafirishwa
kwa matibabu zaidi katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Mjini Dr es
salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi pamoja na wasaidizi wake alipata wasaa wa kufika
Muhimbili kufutilia maendeleo ya afya ya Mtendaji wake Waziri Haroun.
Akimfariji Waziri huyo wa Kazi na
Utumishi wa Umma Zanzibar Balozi Seif alimtakia afya njema na kupona
haraka ili arejee nyumbani kuendelea kutekeleza majukumu aliyokabidhiwa
na Taifa.
Balozi Seif alisema ukimya wa Waziri
Haroun uliokuwepo katika kipindi hichi kifupi katika matukio mbali mbali
ikiwemo Vikao vya Baraza la Mapinduzi umepunguza mchango wake
uliozoeleka ambao hupenda kuutoa mara kwa mara.
Naya kwa upande wake Waziri wa Kazi na
Utumishi wa Umma Zanzibar Mh. Haroun Ali Suleiman ameishukuru Serikali
ya kwa mchango mkubwa iliyoutoa katika kushughulikia afya yake wakati
wote alipokuwa Hospitalini hapo.
Waziri Haroun alielezea faraja yake
kutokana na moyo ulioonyeshwa na Viongozi mbali mbali wa Kiserikali,
Kisiasa wakiongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuamua kumtembelea kujua maendeleo ya afya
yake.
Aliendelea kumuomba mwenyezi Muungu azidi
kuwapa moyo wa huruma na upendo viongozi hao kuzidi kuwa karibu
na wananchi wanaowaongoza katika sehemu mbali mbali nchini.
Post a Comment