Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mawaziri waahidi makubwa

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro akipongezwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (katikati) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam jana. Picha na Emmanuel Herman 
**********
 
Baada ya Mawaziri na Manaibu Waziri kuapishwa jana na Rais Jakaya Kikwete, wametoa ahadi lukuki kwa Watanzania kuhusu utendaji wao.
Mawaziri saba na manaibu mawaziri 11 walikula kiapo mbele ya Rais Kikwete, huku wengine watatu ikielezwa kuwa wataapishwa siku nyingine kutokana na kutokuwapo nchini.
Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yalifanyika juzi ambapo mawaziri watano walitupwa na kuingizwa 10 wapya, kupandishwa manaibu wanne kuwa mawaziri kamili na kuwahamisha wengine wanane kutoka wizara zao kwenda nyingine.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema atafanya kazi kwa jitihada kubwa, uadilifu, ushirikiano na kutoa huduma kwa wakati.
Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM alisema, “Nitafanya kazi kwa jitihada za hali ya juu, uadilifu, ushirikiano na kutoa huduma kwa wakati. Watu wanadhani kuingia Wizara ya Fedha ni kuchota fedha, binafsi nakwenda kusimamia sera”

Alisema moja ya mambo atakayohakikisha kuwa anamshauri Rais Kikwete ni pamoja na kuhakikisha kuwa nchi inaachana na utaratibu wa kuwa na bajeti tegemezi.
“Kuongeza vyanzo vya mapato kutakuja kama ukusanyaji wa kodi unasimamiwa ipasavyo na kupunguza matumizi ya Serikali,” alisema.
Alisema jambo jingine atakalolifanya ni kumshauri Rais kuhusu Sheria ya Ununuzi lengo likiwa ni kuondokana na ununuzi wa vitu mbalimbali kwa mtindo wa zabuni, kwa maelezo kuwa mtindo huo huifanya Serikali kutumia kiasi kikubwa cha fedha.
“Jambo hili la ununuzi ni pana na linahitaji kushauriana na kufanya uchambuzi wa kitaalamu. Pia nitashirikiana na wenzangu kuhusu kuminya mianya mingine inayochangia Serikali kukosa mapato yake ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),” alisema Nchemba.
Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Asha Rose Migiro alisema moja ya majukumu atakayoyafanya ni kuhakikisha kuwa mchakato wa Katiba Mpya unakwenda kama ulivyopangwa, huku akisisitiza kuwa hawezi kukipendelea CCM katika mchakato huo.
“Nitasimamia mchakato wa Katiba katika kipindi hiki ambacho tunaelekea kwenye Bunge la Katiba na baadaye Kura ya Maoni. Jambo zuri ni kwamba mchakato huu unakwenda kwa mujibu wa sheria. Nawahakikishia Watanzania nitafanya kazi kwa uaminifu na kujituma,” alisema Migiro.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufunzi, Jenister Mhagama alisema sekta ya elimu kwa muda mrefu imekuwa na changamoto nyingi na kwamba moja ya mambo atakayoyafanya ni kuhakikisha kuwa anapambana na changamoto hizo.
 
MWANANCHI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top