Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mawaziri wafanya makabidhiano ya wizara ya afya na ustawi wa jamii leo

 


DSC_1613
Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na sasa ni Waziri wa Ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) akizungumza  na watendaji wa wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya ofisi  na aliyekuwa Naibu Waziri wake na sasa ameteulikuwa kushika nyadhifa ya Uwaziri Dkt. Seif Rashid (kulia), anayefuata ni Naibu Waziri wa  Wizara hiyo Dkt. Kebwe S. Kebwe.Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Waziri, wizarani hapo. DSC_1645
Waziri wa  Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Seif Rashid (kulia) akizungumza na watendaji wa wizara hiyo (hawapo pichani) na kutoa shukrani zake za dhati kwa aliyekuwa Waziri wake Dkt. Hussein Mwinyi  kwa ushirikiano wake kipindi alipokuwa akiongoza wizara hiyo. DSC_1660
Naibu Waziri  Dkt. Kebwe S. Kebwe akizungumza na watendaji wa wizara hiyo na kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano na mahusiano mazuri  ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta hiyo

 DSC_1661
Waziri wa Ulinzi Dkt. Mwinyi akiteta jambo na katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jami, Charles Pallangyo. DSC_1670
Naibu Waziri Dkt. Kebwe kulia, akikabidhiwa  kitabu na Waziri Dkt. Mwinyi
DSC_1693
Mawaziri hao wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano pamoja na watendaji wa wizara hiyo. Wa kwanza kushopto waliokaa ni Katibu Mkuu, Charles Pallangyo, aliyekuwa Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt. Mwinyi, Waziri mpya wa wizara hiyo Dkt. Seif nna wa mwisho kulia ni Naibu Waziri Dkt. Kebwe S. Kebwe ( Picha zote na Catherine Sungura-MOHSW)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top