Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini,Mh.Peter Msingwa amefanya mkutano hapo jana katika viwanja vya Mwembetogwa, mkoani humo.
Mkutano
huo ambao ulikuwa wa kufungia mwaka 2013 ,Msigwa pia aliutumia mkutano
huo kwa kuwapongeza baadhi ya mawaziri ambao utendaji kazi wao
unaonekana kuwa mzuri,akiwemo Waziri wa Wizara ya Maji na Naibu Wake
,Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Mazingira ambao wameonesha msimamo wa
kweli katika kuwatumikia wananchi .
katika
hatua nyingine mbunge Msigwa amemshukia aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu
wa Chadema,Zitto Kabwe na kusema kuwa anatafuta umaarufu binafsi
kuliko kukijenga chama chake na kuwa hana nia njema na
CHADEMA,hivyo amewataka Wanachadema wa jimbo la Iringa mjini
kutomsikiliza huku akibainisha kuwa Mwanachama na Kiongozi mzuri ni
yule ambae anafanya kazi ya kukijenga chama chake na si kujijenga
yeye binafsi.
Amesema
kuwa iwapo Zitto hatotaka kumsikiliza mwasisi wa Chama hicho, Mzee
Mtei wala kuwasikiliza viongozi wa juu wa chama hicho akiwemo
mwenyekiti wa katibu mkuu, ni wazi hakitakii mema CHADEMA,na wana
Chadema hawana budi kumpuuza kiongozi na mwanachama yeyote mwenye lengo
la kuua chama.
Kuhusu
rasimu ya Katiba, Mbunge Msigwa amempongeza Rais Kikwete kuwa
ameonyesha ushujaa wa hali ya juu katika kupigania upatikanaji wa
katiba mpya, na kuwa iwapo wabunge wa CCM watapinga wao kama Chadema
watarudi kwa wananchi kuhamasisha kupiga kura ya kuikataa katiba
itakayopendekezwa na wabunge wa CCM.
Aidha
Msigwa ameongeza kusema kuwa atakuwa mstari wa mbele kuikosoa serikali
kama itaonekana kuwa na viongozi dhaifu huku akiwataka watanzania
kutathimini yale yote waliyofanya mwaka 2013 na kuwatakia kheri ya mwaka
mpya.
Post a Comment