Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mbwa Mwitu" sita wafikishwa mahakamani jijini Dar


Wakazi sita wa Dar es Salaam maarufu Mbwa Mwitu au waanzilishi wa kundi la Watoto wa Mbwa, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Sijali Abdallah (19), Sadick Mpambe (25) maarufu Chitemo na Balozi Inasio (19) wote wakazi wa Kiwalani.
Wengine ni Shahibu Japhary (30) maarufu Cardinal Pengo mkazi wa Yombo Kwa Limboa, Mussa Muhunzi (31) maarufu Matikiti na mkazi wa Kiwalani Kijiwesamli na Zegamba Kihongo (20) mkazi wa Kiwalani Migombani.


Katuga alidai mahakamani hapo kuwa, washtakiwa kwa pamoja walitenda kosa hilo Januari Mosi mwaka huu eneo la Yombo Kiwalani, Wilaya ya Ilala.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, washtakiwa kwa pamoja siku ya tukio waliiba Sh150,000 taslimu na simu moja ya mkononi, mali ya Juma Fungo.


Iliendelea kudaiwa mahakamani hapo kuwa, washtakiwa kwa pamoja kabla na baada ya kufanya unyang’anyi huo wanadaiwa walimtishia mlalamikaji kwa panga na kisu ili waweze kupata vitu hivyo kwa urahisi.

Washtakiwa walikana shtaka na Hakimu Wilberforce Luhwago aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 31, mwaka huu itakapotajwa tena.

Washtakiwa walirudishwa rumande kutokana na shtaka linalowakabili la unyang’anyi wa kutumia silaha kutokuwa na dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.

>>Mwananchi
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top