MTOTO
mmoja aliyetambulishwa kwa jina la Joyce Jeremia, 11,(pichani)
amejeruhiwa vibaya katika mapigano ya wa kulima na Wamasai ambao ni
wafugaji katika Kijini cha Laitini, Kiteto mkoani Manyara.
Baba
mdogo wa mtoto huyo Amos Njelu aliwasimulia waandishi wetu akiwa katika
Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi) amesema kuwa mtoto huyo
alijeruhiwa Jumamosi ya Januari 12, 2014 katika kijiji hicho ambacho
kilivamiwa na wafugaji wa Kimasai.
Aliongeza
kusema kuwa baada ya uvamizi huo Wamasai hao walichoma nyuma ambayo
wazazi na watoto akiwemo yeye walikuwa akiishi lakini Wamasai hao
waliweza kufanya mashambulizi na kumuaa baba yake na kumjeruhi mama yake
huku akiona.
“Nilijaribu kumasaidia lakini nikakatwa panga kichwani na mama naye alikatwa mdomo na kukimbia kusikojulikana.
“Hadi
hivi leo sina mawasiliano na mama yangu ambaye alikimbia na wadogo zangu
wawili ambao ni Furaha na Peter,” alisema mtoto huyo.
Mtoto
huyo ambaye alipatwa na jeraha kubwa la kichwa amelazwa Moi katika
Wodi ya watoto na 8 akiendelea na matibabu huku akisaidiwa na baba
yake mdogo pamoja na shangazi yake.
Baba mdogo wa mtoto huyo alisema kuwa lengo la Wamasai hao lilikuwa ni
kuwaondoa wakulima hao ili waweze kuweka mifugo yao kwa ajili ya
kuchungia.
Aliongeza kusema kuwa alikuwa anapata taarifa kutoka kwa majirani kuwa
kaka yake aliyemtaja kwa jina la Kisuligwe Chilongola amefariki dunia
kutokana na vurugu za Wamasai.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, ACP Akili Mpwapwa alikiri kuwepo kwa mapigano hayo ya wakulima na wafugaji.
“Ni kweli
mauaji yalitokea hadi sasa idadi ya waliouawa ni kumi na majeruhi mmoja
lakini kuhusu mtoto huyo hatukuwa na taarifa zake… tunaendelea na
uchunguzi ,” alisema Kamanda Mpwapwa.
Post a Comment