Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MFANYAKAZI WA GEPF DAR AKUTWA AMEKUFA CHUMBANI KWAKE


Mkazi wa Mwenge jijini Dar es salaam Philimon Nelson (45) ambaye alikuwa mfanyakazi wa GEPF amekutwa amefariki akiwa amelala kitandani chumbani kwake, huku mwili wake ukiwa hauna jeraha lolote. 

Kwa mujibu wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam taarifa zinasema kuwa sababu za kifo hicho bado hazijafahamika ingawaje kwa maelezo ya ndugu wa marehemu walidai kuwa marehemu enzi za uhai wake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifafa. 

Na kwasasa maiti imehifadhiwa hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi huku upelelezi ukiendelea. N katika hatua nyingine jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limesema kuwa mnamo januari 19,2014 saa nane kamili mchana maeneo ya Buguruni Kisiwani maarufu kama Msikitini wa Msufini ilikutwa maiti ya mtu mmoja mwanaume aliyetambulika kwa jina la Shabani Rajabu , anayekadiliwa kuwa na umri wa kati ya 35 hadi 40 ambaye ni mfanyabiashara soko dogo la Kariakoo ikiwa imelala maeneo hayo na huku mwili wake ukiwa hauna jeraha lolote.

 Aidha Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limesema kuwa kuhusu tukio hilo kwa mujibu wa mashuda walidai kuwa mtu huyo alikuwa akitembea na ghafla alidondoka chini na kufariki dunia .

Jeshi la polisi kanda maalum ya dar es salaam limeendelea kusema kuwa chanzo chake bado hakijafahamika na maiti imehifadhiwa hospitali ya Taifa Muhimbili.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top