Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

NJEMBA IRINGA MATATANI KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA MIWILI


RPC -Mungi
******
JESHI  la polisi mkoani Iringa linamshikilia Eliabu Myogile (17) mkazi wa Gangilonga kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka miwili.
 
Akizungumza  ofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea tarehe 19 januari mwaka huu.
 
Kamanda Mungi alisema mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto wa kike jina limehifadhiwa na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri, chanzo cha tukio hilo la ubakaji ni tama ya mwili.
 
Mbali na tukio hilo la ubakaji Kamanda Mungi alisema wachumaji wa chai walioajiriwa pamoja na vibarua wa kiwanda cha chai Kilima estate kilichopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa walifanya mgomo na kuharibu mali mbalimbali za kiwanda hicho.
 
Mungi alisema chanzo cha mgomo huo ni wafanyakazi kulipwa mshahara mdogo ambao ulipelekea wafanyakazi hao kuiba mifuko ya saruji na mabati yaliyohifadhiwa stoo, katika tukio hilo hakuna binadamu yeyote aliyedhuhurika.
 
 Credit: Francis Godwin blogMWANDISHI ,DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top