Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MKUTANO WA KITAIFA KUHUSIANA NA KUTOKOMEZA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO WAJA.


 


Taasisi  ya    wanawake  na  maendeleo  (WAMA)   na  Management  Development  For  Health  (MDH)  Tanzania  kwa  kushirikiana  na  wizara  ya  afya   na  ustawi  wa  jamii  itafanya  mkutano  wa  kitaifa  utakaohusu  kutokomeza  maambukizi  ya     virusi  vya  UKIMWI  kutoka  kwa  mama  kwenda  kwa  watoto .

Akizungumza  na  waandishi  wa  habari  jijini  dar  es  salaam  mkurugenzi  wa  idara  ya  uboreshaji  afya  wa   taasisi  ya  wanawake   na  maendeleo  (WAMA)  Dr  Sarah   Maongezi   alisema  kuwa  Mkutano  huo  unataraji    kufanyika  kesho  januari  21 ,2014  jijini  dar  es  salaam  katika  hoteli  ya  Serena  ambapo  mgeni  rasmi  anatarajiwa  kuwa  mheshimiwa  Mama   Salma  Kikwete , mke  wa  Rais  wa  jamhuri   ya  muungano   wa  Tanzania    na  mwenyekiti  wa  Taasisis  ya  wanawake   na  maendeleo  (WAMA)

Aidha   Dr  Maongezi  ameongeza  kuwa    mkutano  huo  utawahusisha  wadau  mbalimbali  kutoka  wizara  ya  afya  na  ustawi  wa  jamii , watendaji   katika  ngazi  ya  serikali  ya  mtaa, mashirika  yasiyo  ya  kiserikali,wadau  wa  maendeleo,wanaoishi  na  maambukizi  ya  WU  na  UKIMWI ,wanataaluma,mashirika  ya  kidini  kwa  pamoja   wote  hao  watashiriki  ili  waweze  kutoa  uzoefu  wao  kuhusiana  na  changamoto  na mikakati   muhimu  katika  kufikia  mafanikio  ya  malengo  ya    mpango   wa  kitaifa.
Pamoja  na  hayo  Dr  Maongezi  alisema  kuwa  ujumbe  mkuu  wa   mkutano  huo  ni  

“Kufanya  kazi   kwa  pamoja  kufikia  lengo  la maambukizi  sifuri  kwa  watoto –Timiza  wajibu  wako”

 Naye  mratibu  wa  huduma  ya  mama  na  mtoto  Dr  Mary  Mwanyika   Sando  kutoka  Management  And  Development  for  Health  (MDH)  alisema  kuwa  wamejikita  sana  katika   kuhakikisha  watoa   huduma  za  afya  wanatoa  huduma    kulingana  na  taratibau  na  miongozo  ya   wizara  ya  afya,  na  hivyo   wanajitahidi  kutoa  msaada  ili  kuhakikisha  wahudumu   wa  afya   wanapata  mafunzo    ambayo  yanaendana  na  miongozo  ya  wizara  ya  afya.

Vilevile   Dr  Mwanyika  amesema  kuwa   Management  And  Development  For  Health   (MDH)   kwa  kushirikiana  na  (WAMA )   wamelenga  kuhakikisha  kweli  Tanzania  bila  Ukimwi,bila  maambukizi  mapya  na  bila  vifo  vitokanavyo  na  ukimwi  au  unyanyapaa  inawezekana  na  hivyo  wamejitahidi  kujikita  katika  mstari  wa  mbele  ili  kuhakikisha  kinamama  pamoja  na  familia  zao   wanapata  hizo  huduma.


Taasisi  ya  Wanawake  na  Maendeleo  (WAMA)  ilianzishwa  mwaka  2006  na  mheshimiwa  mama  Salma  Kikwete , ni  taasisi  isiyo  ya  kiserikali  yenye  lengo  la  kuwaendeleza  wanawake  na  wasichana  wa  kitanzania  hasa  waliotoka  katika  mazingira   hatarishi ,  na  moja  ya  malengo  ya  taasisi  ya  WAMA  ni  kuongeza  fursa  za  elimu  kwa  watoto  wa  kike.
Mwandishi Kenneth John wa matukiodaima.com Dar es Salaam

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top