Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WATATU WAFARIKI DUNIA IRINGA KTK MATUKIO TOFAUTI

 

 
RPC Mungi 
Watu watatu wafariki dunia katika na wengine kumi kujeruhiwa katika matukio mawili tofauti likiwemo la mtoto Yusta Mkonda (10) mkazi wa kijiji cha Migoli mkoani Iringa kutumbukia kisimani.
Akizungumza  ofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea tarehe 17 januari  majira ya saa 12 kamili jioni.
Kamanda Mungi alisema mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Mtera alitumbukia kisimani alipolkuwa akichota maji.

Wakati huohuo watu wawili wafariki dunia na wengine kumi kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepanda kuacha njia na kupinduka maeneo ya kijiji cha Ifwagi wilaya ya Mufindi.

Kamanda Mungi aliwataja marehemu ni Isack Ngozi (25) pamoja na Paul Mbalinga (23) ambao walikuwa wamepanda gari aina ya isuzu forward lenye namba za usajili T 478 ABX mali ya O. Mwidani lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina moja la Nuhu.

Mungi alisema majeruhi kumi waliokuwemo katika gari hilo walilazwa katika Hospitali ya Mafinga huku dereva wa gari alikimbia mara baada ya ajali.
MWANDISHI ,DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top