Na John Joseph
ALIYEJITANGAZA kuwa
mmiliki wa klabu ya Yanga, Juma Mwambelo, amesema yu tayari kukabidhi
nyaraka zinazotafutwa na uongozi wa klabu hiyo kwa Rais wa Tanzania,
Jakaya Mrisho Kikwete.
Makamu
Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, alitangaza kwenye mkutano wa Yanga
kwamba Mwambelo anashikilia hati za umiliki wa klabu ya Yanga kimakosa
na anatakiwa kuzikabidhisha haraka iwezekanavyo kabla ya kuchukuliwa
hatua.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Mwombelo alisema yupo tayari kumpa Rais
Kikwete naye aukabidhi uongozi wa Yanga chini ya Yusuf Manji.
“Kweli
hati hizo ninazo kwa kuwa mimi ni mmiliki wa Klabu ya Yanga, ila Rais
Kikwete pekee ndiye naweza kumkabidhi, hata mwanaye Ridhwani nimewahi
kumueleza kuhusiana na hili,” alisema.
“Mimi
ndiye mmiliki wa Klabu ya Yanga, nina hati miliki halali ya klabu, hii
hapa (anaonyesha), nina hati miliki ya jengo la Jangwani, pia ninayo ya
jengo la Mafia, lakini hiyo waliiba na tayari nilisharipoti polisi.
“Kuhusu
hati ya jengo la Jangwani ipo benki na yenyewe sijailipia kwa kuwa kuna
deni, deni hilo ni zile fedha ziliyotumika kujenga Uwanja wa Kaunda.
Hivyo,
deni likilipwa benki itakubali kutoa hati kisha kuirudisha wizarani na kutolewa rasmi.
“Nashangaa
Yanga wanapodai wanatumia katiba mpya, hii siyo halali, katiba halali
ya Yanga ni ile ya mwaka 1967 ambayo nakala yake hii hapa (anaonyesha),”
alisema.
Alipoulizwa
juu ya uhalali wa wanachama wa sasa wa klabu hiyo, alisema: “Wanachama
wengine wote ni feki, mpaka unatokea mgawanyiko mwaka 1975, wanachama
halali wa Yanga walikuwa 400, kuanzia hapo hakuna wanachama halali tena,
hata akaunti zinazotumika siyo za klabu.
“Hapa
nilipo nimekuja polisi (Magomeni) ili kutoa taarifa ya kujihami, nahofia
kupigwa kutokana na walichokisema kwenye mkutano,” alisema.
Katika
mkutano mkuu wa Jumapili, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Karume, PTA
Sabasaba jijini Dar es Salaam, uongozi wa Yanga ulimtaja mzee Juma kuwa
ndiye aliyeiiba hati ya jengo la klabu hiyo tangu Juni 24, 2009.
“Mimi
nilipigwa na watu mwaka 1987 nikapoteza fahamu kwa siku tano, tangu pale
sijawahi kwenda klabuni wala uwanjani kuitazama Yanga, hata huyo Mrisho
Ngassa simjui, namuona tu kwenye magazeti, kikubwa ninachotaka ni
utaratibu ufuatwe ndani ya Klabu ya Yanga,” alisisitiza huku
akitabasamu.Credit: GPL
Post a Comment