Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MREMA CUP 2014 YAZINDULIWA RASMI

 


SAMSUNG CAMERA PICTURES
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Dkt. Augustino Mrema akikabidhi jezi kwa
viongozi wa vilabu 15 vitakavyoshiriki mashindano ya Mrema Cup 2014,
katika hafla ya uzinduzi uliofanyika juzi katika uwanja wa Himo. Picha
na Taifa Letu.com Blog
SAMSUNG CAMERA PICTURES
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Dkt. Augustino Mrema akikagua wachezaji wa
klabu ya Himo na Njia panda katika mechi ya uzinduzi wa Mrema Cup
2014, uliofanyika juzi katika viwanja vya Himo, wilaya ya Moshi,
mkoani Kilimanjaro. Picha na Taifa Letu.com Blog
SAMSUNG CAMERA PICTURES
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Dkt. Augustino Mrema akikabidhi jezi kwa
viongozi wa vilabu 15 vitakavyoshiriki mashindano ya Mrema Cup 2014,
katika hafla ya uzinduzi uliofanyika juzi katika uwanja wa Himo. Picha
na Taifa Letu.com Blog

………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Moshi
MBUNGE wa Jimbo la Vunjo (TLP), Dk. Augustino Mrema, amezindua
mashindano ya soka, Mrema Cup 2014, yatakayoshirikisha jumla ya vilabu
15 kutoka katika kata zote 15 ya jimbo hilo.
Akizungumza na Tanzania Daima mara baada ya uzinduzi huo, Dk. Mrema
alisema lengo la mashindano hayo ambayo ni ya kwanza kufanyika jimboni
hapo ni kutoa fursa za ajira kwa vijana pamoja na kuleta mshikamano
katika jamii.
Dk. Mrema alisema kwa sasa hakuna sekta inayofanya vizuri katika kutoa
ajira kwa vijana kama michezo huku akisistiza umuhimu wa kushiriki
michezo kwa lengo la kuhamasisha Amani, mshikamano na umoja katika
jamii.
“Tunazindua mashindano haya kwa lengo moja tu, kuhamasisha mshikamano,
amani na udugu wetu, dunia nzima hakuna sekta inayochangia kutoa fursa
za ajira kama michezo hasa mchezo wa soka, vijana wakishiriki michezo
wanapata kazi lakini pia inasaidia kuimarisha Afya,” alisema Dk. Mrema
Naye, Mratibu wa Mashindano hayo, inspecta msaidizi wa polisi kituo
cha himo, Laban Sospeter alisema, Vilabu vitakavyoshiriki katika
mashindano hayo ni Himo, Njia panda, Kahe, Makomu, Mamba, Kilema,
Mandaka, Riata, Makuyuni, Mitsubishi na Kifaru ambayo ni timu
mwalikwa.
Laban alisema baada ya uzinduzi huo, wanatarajia kuanza mashindano
hayo wiki ijayo ambapo katika mechi ya uzinduzi kati ya Njia panda FC
na Himo SC ulishuhudia Njia panda wakiibuka na ushindi wa 1-0.
Zawadi zitakazotolewa kwa washindi ni shilingi laki tano kwa mshindi
wa kwanza, mshindi wa pili ni shilingi laki tatu na mshindi wa tatu
akiondoka na laki mbili fedha taslim ambapo jumla ya shilingi milioni
moja zita zitashindaniwa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top