***
MSICHANA mwenye umri wa miaka 10
aliyejulikana kwa jina mola la Spozhmai, nchini Afghanistan, anayedaiwa
kutaka kujilipua kwa mabomu mbele ya kituo cha polisi, amekamatwa.
Akizungumza na waandishi wa habari huko
Lashkar Gah, mji mkuu wa jimbo la Helmand, Spozhmai alidai kwamba kaka
yake ambaye ni kamanda wa wapiganaji wa Taliban alimlazimisha kuvaa
koti maalum la kubebea mabomu na kumtaka aende kwenye kituo kimoja cha
polisi akajilipue.
Aliendelea kusema kwamba baada ya
kumsimulia kaka yake juu ya kuchoshwa na vituko vya mama yake wa kambo
dhidi yake, kaka yake huyo alimshawishi avae mabomu hayo aende kwenye
kituo cha polisi cha wilayani Khanashin, kusini mwa nchi hiyo na
abonyeze kidude cha kuyalipua.
“Nilivuka mto mmoja na baadaye nikaamua
kulivua na kulitupa koti hilo. Kaka yangu alikimbia na polisi
wakanikamata,” alisema msichana huyo.
Habari kutoka televishni ya Tolo zimesema
kilichokuwa kimetokea ni kwamba msichana huyo alishindwa kukibonyeza
kidude cha kuyalipulia mabomu hayo.
Kumekuwa na habari kwamba Taliban wamekuwa
wakiwatumia watoto katika kuweka mabomu kando ya barabara na kwa
kujilipua, jambo ambalo wapiganaji hao wamelipinga.
NA: SKY NEWS
Post a Comment