MTIBWA Sugar imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba
kwenye mchezo wa kirafiki kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Soka ya
Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa leo.
Simba walikuwa wa kwanza kubisha hodi kwenye lango la Mtibwa
Sugar kwenye dakika ya 12 lakini shuti la mshambuliaji mpya wa timu hiyo Ally
Badru liliishia mikononi mwa kipa Hussein Sharif. Kabla ya kupiga shuti hilio
dhaifu Badru alikuwa amepata pasi ya Said Ndemla.
Mtibwa Sugar walijibu mapigo kwenye dakika ya 25 lakini
mshambuliaji wake Jamal Mnyate alikosa bao la wazi kwa shuti alilopiga kutoka
pembeni kidogo ya lango la Simba.
Timu hiyo kutoka mkoani Morogoro ilitawala sehemu kubwa ya
kipindi cha kwanza nusura wapat bao kwenye dakika ya 27 lakini beki wa Simba
Gilbert Kaze aliokoa mpira uliokuwa unatinga wavuni wa mshambuliaji Masoud
Ally.
Simba walifanya shambulizi la kushtukiza lakini mshambuliaji
wake Betram Mwombeki alipoteza nafasi nzuri ya kufunga kwenye dakika ya 33 akiwa peke yake na goli lakini
shuti lake lilitoka pembeni kidogo ya lango la Mtibwa Sugar.
Dk 46 Simba walifanya mabadiliko kwa kuwaingiza Nassoro
Masoud’Cholo’ na Adyoun Saleh badala ya Omary Salum na Wiliam Lucian huku
Mtibwa wakifanya mabadiliko kwa kumuingiza Vicent Barnabas badala ya Ally
Mohamedi aliyeumia.
Dk 53 Mtibwa Sugar walipata pigo baada ya mchezaji wake
Salim Mbonde kutolewa nje baada ya kugongana na kipa wake Hussein Shariff na
kulazimika kubebwa kwa machela kupelekwa chumba maalumu cha matibabu.
Dk 65 Ally Masoud aliifungia Mtibwa Sugar bao la kuongoza
baada ya kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Hussein Ramadhani.
Vikosi Simba Yaw Berko. Wiliam Lucian, Omary Salum, Kaze
Gilbert, Donald Musoti, Awadh Juma, Ramadhani Chombo, Edward Cristopher, Betram
Mwombeki, Ally Badru na Saidi Ndemla.
Mtibwa Hussein Sharif, Said Mkopi, Paul Ngalema, Salim
Mbonde, Salvatory Ntebe, Shaabani Nditi, Ally Shomary, Masoud Ally, Juma
Luizio, Jamali Mnyate.CHANZO http://pallangyor.blogspot.com/
Post a Comment