Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mwenyekiti wa Chadema Temeke apigwa na kuumizwa vibaya na kisha kutupwa Dar usiku kuamkia leo ... Tazama hali yake ilivyo, inatisha

 ununio8
 
ununio1
 
ununio6
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Temeke Joseph Yona amepigwa na watu wasiojulikana na kisha kutupwa kwenye eneo la Ununio kwenye Magorofa ya Wasomali Kawe Dar es salaam.
Shuhuda Abdul Ally ambae ni mkuu wa nyumba zilizokaribu na alikopigwa Mwenyekiti huyu, anasema walisikia kelele za huyu mtu kupigwa saa tisa usiku na walipomsogelea walimkuta peke yake.
‘Niliomba wasiniue, wamenipiga sana… wamenichukua saa tano nyumbani kwangu Kwa Aziz Ally, wao walikua na gari kama ya Polisi lakini inaonekana sio ya polisi wakasema tunakupeleka Central, tulikua wanne na hawakuhangaika na mtu wakanichukua mimi moja kwa moja.. tulipopanda kwenye gari wakachukua nguo yangu wakanifunga uso, wakaanza kunipiga wakisema nisiwajibu na hawakuniambia chochote’
Unaweza kusikiliza maelezo yake mengine akihojiwa kwa kubonyeza play hapa chini..
 


ununio7
ununio6
ununio5
ununio4
ununio3
ununio1
DSC_0027
ununio2
        Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa temeke bw. Yona amepigwa na kuumizwa vibaya Leo usiku na kutupwa maeneo ya ununio. Yona amekuwa ni akipinga vikali maamuzi ya kamati kuu CHADEMA kuwavua uanachama dkt Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba na Zitto Kabwe. katika sakata linaloendelea CHADEMA. Huyu ni mwanachama wa 3 kukumbwa na kipigo baada ya katibu wa mbunge dkt Alex kupigwa maeneo ya tegeta, mjumbe wa kamati kuu kupigwa ndani ya kikao na sasa mwenyekiti huyu wa temeke. Kabla ya hapo Samson Mwigamba alipigwa mbele ya mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe.
Baada ya kushindwa hoja uongozi wa chadema umeamua kutumia mabavu na kujeruhi watu wanaopingana nao kimawazo.

millard ayo

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright 2025 EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG | Designed By Code Nirvana