MFUKO WA PENSHENI WA (PSPF)
SALAMU ZA PONGEZI
Waziri wa Fedha Mhe.
Saada Mkuya Salum (MB)
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mh. Adam K. Malima.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na wafanyakazi wa Mfuko wa
Pensheni wa PSPF wanatoa pongezi za dhati kwa Mhe. Saada Mkuya Salum (MB) kwa
kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.
Vile vile, PSPF inatoa pongezi kwa kuteuliwa kwao Naibu Mawaziri wapya wa
Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba (MB) na Mh. Adam K. Malima.
Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wote wamepokea kwa furaha
uteuzi wenu mliopewa na Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. PSPF ipo tayari wakati wote kushirikiana
nanyi katika kuleta tija katika utendaji wa Wizara ya Fedha na sekta nzima ya
Hifadhi ya Jamii kwa ujumla hapa nchini.
PSPF - Tulizo la Wastaafu
Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni - PSPF
Post a Comment