ZIARA ya Rais wa TFF Jamal malinzi hatimaye imemelizika leo hapa jijini Mwanza kwa matukio mawili makubwa kufanyika.
Tukio
la Kwanza limefanyika majira ya saa 2:30 katika ofisi za Halmashauri ya
jiji la Mwanza ambapo Shirikisho hilo limesaini mkataba kati yake na
Halmashauri hiyo kwaajili ya kuboresha uwanja wa Nyamagana.
Ili
ipate kumwaga fedha zake za msaada kiasi cha dola laki 5 ambapo nyingine
dola laki 1 zitatoka Halmashauri ya jiji la Mwanza, FIFA ilikuwa
ikitaka uthibitisho toka TFF kuwa uwanja huo kwa miaka yote utatumika
kwa matumizi ya michezo yaani soka na si vinginevyo kwaajili ya kuanza
uboreshaji wa uwanja huo uliokuwa na utata wa kutaka kubadilishwa
matumizi.
Tukio
la pili Malinzi na timu yake ya wataalamu toka TFF, majira ya saa 4
asubuhi imetembelea na kukikagua kituo cha elimu na soka cha Alliance
Academy ikiwa ni mwanzo wa mpango wa kitaifa wa kuwekeza katika soka la
vijana. BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAARIFA KAMILI.
Rais
wa TFF Jamal Malinzi (katikati mwenye miwani) akiwa ameongozana na
Mkurugenzi wa kituo cha Elimu na Ukuzaji vipaji vya michezo cha Alliance
Academy James Bwire (kulia) akikagua mabweni ya wavulana ya kituo.
|
Rais
wa TFF Jamal Malinzi (wa pili kutoka kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa
Chama Cha soka mkoa wa Mwanza (MZFA) Jackson Songora (wa kwanza
kushoto), mkurugenzi wa kituo hicho James Bwire (wa tatu kutoka kushoto)
pamoja na mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa kitengo cha michezo
(kushoto) wakifurahia jambo ndani ya moja kati ya mabweni ya wavulana
Alliance Academy.
|
Msafara wa rais huyo pia uliambatana na wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya habari.
|
Vijana wetu hulala hapa.
|
Bweni vyumba baada ya vyumba.
|
Tofauti
na eneo la kukaa watazamaji kwa kila kiwanja, katika eneo hili
vimeunganika viwanja viwili vyenye ukubwa wa mita 100 kila kimoja
(nazungumzia maeneo ya kuchezea) na kingine kilichopo eneo la mabweni ya
wasichana, ambapo TFF kupitia rais wake Jamal Malinzi imeahidi
kuvikarabati viwanja hivi kwa kuvisawazisha kwa greda, kuviwekea magoli
ya kisasa, kuweka udongo wenye rutuba na kuviwekea nyasi za kupanda
zenye kiwango.
|
Shule
ya Alliance Academy imeongeza eneo hili lenye ukubwa wa hekta takribani
600 ambapo kunajengwa vyumba vya madarasa, ukumbi wa mikutano na ofisi
kwa walimu.
|
Ujenzi ukiendelea ukumbi wa mikutano.
|
Majadiliano.
|
Hili ni eneo jingine na majengo haya ni mabweni ya wasichana Shule ya Secondary Alliance Academy Mwanza.
|
Msafara
umefika hapa katika kiwanja cha soka wasichana ambapo ni moja kati ya
viwanja vitakavyo kutana na mpango wa maboresho wa TFF utakao anza
haraka wiki chache zijazo.
|
Rais
wa TFF Jamal Malinzi (kulia) hapa alikutana na Mwakilishi wa vilabu
mkoa wa Mwanza ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Kariuwa ya
mkoani Tabora, John Kadutu (kushoto) ambapo walikumbushana mambo mawili
matatu na kufurahi kwa pamoja.
|
Jamal
Malinzi alipata fursa ya kuzungumza na wachezaji na wanafunzi vijana
wanaochukua masomo ya usimamizi na uamuzi wa michezo (marefa), kikubwa
sanjari na kuzingatia michezo pia alisisitiza kuiweka elimu mbele.
|
Jiografia kuelekea ofisi kuu za kituo.
|
Katibu
mkuu wa Alliance School Sports Academy (ASSA) Bi. Mariam D. Lima
akisoma risala mbele ya rais wa TFF Jamal Malinzi na wajumbe wake walio
hudhuria ziara ya rais huyo shuleni hapo.
|
Moja kati ya Madhumuni ya kuanzishwa kwa kituo hiki ni pamoja na:-
1. Kujenga,
kuimarisha, kuelimisha na kukuza vipaji vya vijana wa kike na wakiume
katika michezo mbalimbali na kukuza michezo hiyo kwa manufaa yao na
watanzania kwa ujumla.
2. Kuanzisha,
kuendesha na kuendeleza vituo vya michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na
semina na makongamano kwa vijana hapa nchini Tanzania.
3. Kuandaa mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
4. Kuwajengea vijana uwezo wa kujiamini kwa kuwapa maandalizi bora kimichezo na kitaaluma katika kufikia lengo lililokusudiwa.
LENGO KUU / MAHUSUSI
Kuhakikisha kuwa kituo kinakuwa bora na mfano wa kuigwa Afrika.
Katibu
mkuu wa Alliance School Sports Academy (ASSA) Bi. Mariam D. Lima
akimkabidhi risala rais wa TFF Jamal Malinzi mbele ya wadau
waliohudhuria ziara ya rais huyo shuleni hapo.
|
Rais
wa TFF Jamal Malinzi akimkabidhi mpira Captain wa Mwanza Starehe Club
ambaye pia ni mwenyekiti wa uwanja wa CCM Kirumba John Tegete.
|
Pia Rais wa TFF Jamal Malinzi alikabidhi mipira 10 kwa Katibu mkuu wa Alliance School Sports Academy (ASSA) Bi. Mariam D. Lima kwaajili ya matumizi ya kituo.
|
Picha ya pamoja.
|
Post a Comment