WILAYA YA CHUNYA – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 00:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IGUNDU, KATA YA SANGAMBI, TARAFA YAKIWANJA,
WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. PAUL S/O MWASHEMELE, MIAKA 57,
MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IGUNDU ALIFARIKI DUNIA WAKATI
AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU NYUMBANI KWA NDUGU ZAKE. CHANZO NI BAADA
YA KUCHOMWA KISU TUMBONI TAREHE 01.01.2014 MAJIRA YA SAA 12:00HRS
NYUMBANI KWA NGANGA S/O NYAPINI, MIAKA 48, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA
KIJIJI CHA IGUNDU BAADA YA KUMFUMANIA UGONI AKIWA NA MKE WAKE. MAREHEMU
ALIENDELEA KUPATA MATIBABU KWA NDUGU ZAKE MPAKA ALIPOFARIKI DUNIA.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA TAREHE 02.01.2014 NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA
LA SHAMBULIO DHIDI YA MKE WAKE AITWAE TUMAIN D/O LUSAMBA, MIAKA 43,
KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IGUNDU, MTUHUMIWA YUPO GEREZANI
RUANDA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO JAMII KUACHANA NA TAMAA ZA KIMWILI
KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA NA BADALA YAKE WATAFUTE MPENZI MMOJA WA
KUISHI NAE.
WILAYA YA MBEYA MJINI – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 06:00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA RUFAA
JIJINI MBEYA, STEPHEN S/O PHILIPO,MIAKA 28,MSAFWA,MKULIMA,MKAZI WA
KIJIJI CHA NSUNGWI JUU ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA
MATIBABU. MAREHEMU ALIPIGWA KITU KIZITO KICHWANI NA KAKA YAKE LUCAS S/O
PHILIPO,MIAKA 25, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA NSONGWI JUU
TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 05:10HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NSONGWI
JUU KATA YA NSONGWI, TARAFA YA TEMBELA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI.
CHANZO NI UGOMVI WA MASHAMBA BAINA YA WANANDUGU HAO. MTUHUMIWA
AMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI
WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUTATUA MIGOGORO YAO
YA KIFAMILIA KWA NJIA YA AMANI KWA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO ILI
KUFIKIA MUAFAKA.
WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA BAISKELI NA
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 09:45HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
CHAMSALAKA, KATA YA CHIMALA, TARAFA YA ILONGO, BARABARA YA MBEYA/NJOMBE
WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. GARI T.265 BKG AINA YA M/FUSO BASI
LIKIENDESHWA NA DEREVA ZUNDA S/O ERICK, MBUNGU, MKAZI WA MBEYA
LILIMGONGA MPANDA BAISKELI DAUD S/O MWAMBENE, MIAKA 53, MNDALI, MKAZI WA
RUAHA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI MWENDO
KASI. DEREVA ALIKIMBIAMARA BAADA YA TUKIO NA KULITELEKEZA GARI. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA
MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE
MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.
MNAMO
TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 21:25HRS HUKO ENEO LA SOKOMATOLA, KATA
YA SISIMBA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, MTU MMOJA AITWAYE
MARRY D/O ABRAHAM, MIAKA 24, KYUSA, MKULIMA NA MKAZI WA SOKOMATOLA
ALIKAMATWA AKIWA NA FEDHA ZIDHANIWAZO KUWA NI BANDIA NOTI 07 @ TSHS
10,000/= ZIKIWA NA THAMANI YA TSHS 70,000/=. MTUHUMIWA ALIKAMATWA BAADA
YA KWENDA KWENYE KIBANDA CHA M-PESA CHA GRACE D/O STEWART, MIAKA 24,
KYUSA, MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MAJENGO NA KUTAKA KUZIHIFADHI FEDHA
HIZO KWENYE SIMU YAKE. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWEMAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA
WAFANYABIASHARA KUWA MAKINI NA MATAPELI NA KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA
MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA DHIDI
YAO ZICHUKULIWE.
[AHMED.Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment