Hii dimbwi ambalo maji yametuama na kutunza uchafu
Barabara iendayo kutokea uwanja wa zamani wa ndege mbeya ukiwa umejaa maji
Maji yakiwa yamezunguka stoo za wafanya biashara eneo la viwanda sido
Hapa kidogo ni afadhali kuliko maeneo mengine
Hili eneo ndio krofi sana kwa kuwa hujaa sana maji na matope hivyo kusababisha magari kukwama kwa wingi na kuleta usumbufu.
Hapa ndio hapapitiki kabisaaaaaa,ni bwawa la samaki
Kwa mbali nafaka zikiwa zimetunzwa huku maji yakiwa yamezunguka eneo hilo

Barabara ikiwa tope tupuuu hivyo kufanya ushushaji wa nafaka kuwa mgumu
Hali ya barabara katika eneo la sido mkoani Mbeya ni ya kutisha na
kuhuzunisha sana.Eneo hilo ambalo limetengwa maalumu na Jiji la mbeya
kwa ajili ya stoo za wafanyabiashara na pia ni maalumu kwa watu
wanaohusika na ukoboaji,usagaji na kukamua mafuta ya alizeti.Ukifika
eneo hilo kipindi cha kiangazi huwa ni kavu lakini kuna mashimo mengi
yasiyorekebishwa.
Shida huwa inakuja kipindi cha masika na mvua nyingi ambapo
kupitika kwa maeneo yanayozunguka eneo hilo huwa ni shida sana kwa
waenda kwa miguu na pia magari makubwa na madogo yanayoshusha na kupakia
mizigo kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania.
Eneo hili pia ni kiungo muhimu sana kwa wakazi wanaokaa maeneo ya
uwanja wa ndege,kwa kuwa wengi wanatumia njia hii kama ni shortcut ya
kufika haraka majumbani mwao.Dj sek blog ilifanya uchunguzi yakinifu kwa
takribani wiki moja eneo hili na kuweza kuvumbua mambo mengi sana,Moja
ya mambo hayo ni kwamba kwa kiasi kikubwa eneo hili hutumika kama makazi
yasiyo rasmi kwa watoto wa mitaani,ambao wengi hawana makazi au mahala
pa kulala.
Watoto hao wa mitaani hutumia majengo ambayo hayajamalizika vizuri
kujiihifadhi kama makazi yao,Mtandao wetu ulifanya mahojiano na baadhi
ya wamiliki wa mashine na stoo za eneo hilo kubwa ni kutaka kujua
kwanini eneo hilo limetawaliwa na madimbwi,mashimo makubwa na maji
yaliyotuama kwa wingi.Wafanyabiashara hao wameitupia lawama uongozi wa
jiji kwa kushindwa kusimamia vizuri eneo hilo ambalo limetengwa maalumu
kwa ajili yao,wakiongeza kuwa wanatoa kodi kila mwaka,kila mwezi
walitegemea kodi zao zitatumika kukarabati eneo hilo lakini kinyume
chake imekuwa ni shida kwao.
Wafanyabiashara hao wameeleza kuwa mgari yanayokuja kushusha na
kupakia yamekuwa yakipata sana shida kupita eneo hilo hasa kipindi kama
hiki cha mvua,hivyo wameiomba Serikali kuwasaidia kukarabati eneo hilo.
Mtandao
huuu ulijaribu kumtafuta mtu anayeratibu na kusimamia eneo hilo lakini
mpaka tunamaliza utafiti huu hatukuweza kumpata.Rai ya mtandao wetu ni
kwamba viongozi msikae tu huko maofisini tokeni nje pia huku muone
wanaicni wanavyokuwa na kero nyingi. PICHA NA HABARI KWA HISANI YA DJ SEK BLOG
Post a Comment