Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamanda Mkadam Khamis Mkadam |
Siku
ya tarehe 13/01/2014 majira saa 9:55 jioni hapo Rahaleo kwa Mchina Tambi
palitokea tukio la unyangani wa kutumia silaha. Tukio hili lilitokea
wakati Bw: SAID SEIF SALAMI 34, Riami wa RAHALEO ambaye ni MFANYA
BIASHARA wa vyakula anayefanyia biashara yake Kibanda Maiti na anaishi
mtaa wa RAHALEO alipofanyiwa unyanganyi huo.
Mfanya
biashara huyu alifunga biashara yake majira ya saa 9:45 jioni ya siku
hiyo ya tarehe 13/01/2014 na kuchukua pesa za mauzo ya kutwa jumla ya
T.sh 11,500,000/= ambazo alizifunga katika bahasha /mfuko wa kaki na
kuondoka nazo kuelekea nyumbani kwa kutumia gari yake no. Z. 128 EW
NISSAN Rangi ya silver. Alipofika maeneo ya Raha Leo Kwa Mchina Tambi
ndipo gari moja yenye no. Z.866 EX aina ya SCUDO ilipomzinga kwa mbele
na ghafla aliona watu watatu wametokezea wakiwa na silaha mbili, moja
ikiwa ni bastola na nyengine ni SMG. Watu hao walimlazimisha kwa
usalama wake awape ule mfuko wenye pesa. Kwa kuhofia usalama wake alitoa pesa zote jumla ya T.SH 11,500,000/=
Majambazi
hao baada ya kitendo hicho cha kuchukua hizo pesa walikimbilia kwenye
gari yao. Kitendo hicho kilifanyika mbele ya watu ambao walianza kupiga
kelele za mwizi!, mwizi!, mwizi!, kelele ambazo zilimfanya dereva wa
gari ya majambazi kuondosha gari na kuwaacha wenzao watatu chini.
Wakati huo wananchi walipiga simu Polisi huku juhudi za ukamataji zikiendelea.
Polisi
walifika eneo la tukio na kumkuta mtuhumiwa mmoja asiye na silaha akiwa
tayari amekamatwa kwa msaada wa wananchi. Mtuhumiwa huyo anaitwaMAULID
ALI @ KIPARA. Juhudi ziliendelea kufanywa kuwafuatilia majambazi wengine
walioondoka eneo la tukio na silaha. Miongoni mwao jambazi mmoja
alifanikiwa kuitupa silaha aina ya SMG isiyo na magazine na shuka la
kimasai ambalo alikuwa amevaa Jambazi huyo kujaribu kubadilisha
utambulisho wake. Silaha na shuka hilo la kimasai vilitupwa hapo eneo la
ndani ya msikiti wa Muembe Shauri. Jambazi huyu aliruka ukuta na
kutokomea upande wa pili.
Mtuhumiwa
wa tatu aliyekuwa na pistol alikabiliwa na Wananchi wa maeneo ya Kwa
Ali Natoo kwa kushirikiana na Askari wetu wa vyombo mbalimbali wakiwemo
Polisi, KMKM, JKU na Mafunzo na walifanikiwa kumkamata akiwa na hiyo
Pistol aina GLOCK 17 ikiwa na no. PPG 617 ikiwa na risasi zake17 ambayo
alikamatwa nayo Mtuhumiwa huyo aitwaye GANGIRA CHARLES MSHANDETE 34,
MSUKUMA WA DSM anayesadikiwa kuwa ni mtumishi wa PCCB DSM kutokana na
maelezo yake lakini pia kitambulisho na silaha yake vinaonyesha
kumilikiwa na Taasisi hiyo.
Baada
ya mahojiano kuanza, mtuhumiwa wa kwanza alitowa ushirikiano wa namna ya
kumpata mshirika wao ambaye aliendesha gari la Majambazi, hivyo
Mtuhumiwa huyo dereva alikamatwa maneo ya Shangani nyuma ya African
House nyakati za Magharibi. Mtuhumiwa huyo wa tatu anaitwa KHAMIS FAKI
HAJI 40, MSHIRAZI WA MWERA. Baadaye Mtuhumiwa huyo alitoa ushirikiano wa
kuitoa gari iliyofanyia tukio ambayo tayari alikuwa ameshaificha ndani
ya eneo la viwanda vidogo vidogo. Gari hiyo ina no. Z 866 EX aina
ya SUZUKI ambayo ndiyo iliyotumika katika ujambazi.
Baada
ya kukamatwa dereva huyo, mtuhumiwa wa kwanza aliendelea kutoa
ushirikiano kwa kumvuta mtuhumiwa aliyeitupa Bunduki ya SMG pale
msikitini Muembe Shauri. Ilipendekezwa itumike gari ya mtuhumiwa wa tatu
ili kumfanya yule anayevutwa asishituke. Wapelelezi na Mtuhumiwa wa
kwanza walienda hadi eneo walilokubaliana kukutana. Walipofika pale na
ishara ilitolewa ili afike, lakini wakati unafunguliwa mlango wa gari
alibaini kuwa waliokuwemo ni Askari na hivyo alitimka mbio. Juhudi
zilifanyika na akakamatwa. Mtuhumiwa huyo wanne anajulikana kwa jina
la RAJAB MOHAMED BAKAR 25, MSHIRAZI WA KOROGWE TANGA. Licha ya mtuhumiwa
huyu kujitambulisha kwa jina hilo wenzake wanamtambua kwa jina
la CHRISTOPHER MKAAZI WA KIGOMA – MUHA. Mtuhumiwa huyu alipopekuliwa
alipatikana na silaha nyingine ya Pistol aina ya Browning yenye namba TZ
CAR 93480. Hizi ni namba mpya za silaha ambazo kupitia data base ya CAR
DSM tunaweza kujuwa mmiliki halali wa silaha hii na jinsi gani imetoka
mikononi mwake pengine inawezekan na yeye akawa ni mshiriki wa kosa la
ujambazi. Pia pistol hiyo ilikuwa na risasi moja.
Kwa ufupi katika tukio hili silaha zilizokamatwa ni tatu ikiwemo SMG moja na pistol mbili na risasi 18 jumla.
Kuhusu
mali zilizoibiwa pesa taslim T.sh 3,900,000/= zimepatikana na kwamba
mtuhumiwa wa pili ndiye aliyekamatwa nazo pamoja na simu ya mlalamikaji,
kadi ya Benki na leseni ya udereva. Katika sakata la ukamataji
Mtuhumiwa huyu aliutupa ule mfuko wa pesa na mtoto mmoja aliuchukua na
kukimbia nao. Juhudi zilifanywa na akapatikana akiwa ameshawakabidhi
kaka zake ambao walirejesha jumla ya T.sh 3,900,000/= huku mfuko
uliokuwa umehifadhi ukiwa umechanwa hali ya kuwa awali walipokabidhiwa
na huyo mtoto mfuko huo ulikuwa umefungwa vizuri. Mtu mmoja anashikiliwa
kuwezesha upatikanaji wa mali zilizobakia. Kwa jumla walikamatwa watu
saba na kuhojiwa katika tukio zima.
Sambamba
na taarifa hiyo napenda pia kuwaonyesha bunduki aina ya Gobore
tuliyoikamata tarehe 03/01/2014 saa 1:00 usiku huko Fuoni Mkoa wa
Kusini Unguja pamoja na watuhumiwa watatu ambao walikuwa wanajiandaa
kufanya ujambazi kwa BAKHRESA Mtoni Unguja walikamatwa wakiwa na silaha
hiyo ya Gobore yenye kutumia risasi za Shortgun
Watuhumiwa hao ni
Watuhumiwa hawa leo tarehe 16/01/2014 tumawapeleka Mahakamani.
Naomba
kutumia nafasi hii kwa mara nyengine tena kuwashukuru na kuwapongeza
wananchi wote kwa ushirikiano wao katika mapambano na majambazi
tuliofanikiwa kuwakamata tarehe 13/01/2014.
Tunawaomba
wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi lao la Polisi kwa kutoa taarifa
zitakazoweza kusaidia kuwakamata wahusika wa matukio kama haya ambao
lengo lao ni kujipatia mali kwa njia ya mkato lakini pia kuleta hofu na
taharuki kwa wananchi.
Nawashukuru, Asanteni sana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi
Mkadam Khamis Mkadam
Post a Comment