Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
JIJI
la Dar es Salaam nchini Tanzania ni moja ya majiji maarufu ambalo
limepata nafasi ya 39 katika majiji ambayo watu mashuhuri na watalii
wanaweza kutembelea duniani.
Ni
majiji makubwa yenye mageuzi ya muonekano na vitu vya kale vya kuvutia
pamoja na wanyama wazuri na madhari ya kipwani inayoweza kumvuta mtalii
kutoka kokote duniani.
Dar
es Salaam ilipata nafasi ya 39 katika sehemu moja tulivu katika pwani ya
Afrika Mashariki na mji mzuri kwa ajili ya biashara.
Tanzania
inaweza kuwa imejulikana kwa sababu ya mlima Kilimanjaro na mabonde na
milima ya kuvutia bila kusahau mbuga ya wanyama Serengeti.
lakini mapigo halisi ya nchi hupatikana katika mji wake mkubwa, na ndiyo maana Dar es Salaam ikapata nafasi ya 39 duniani.
Watafiti
wa mambo ya kale na utalii wanasema taarifa hiyo ya gazeti la New York
Times la Marekani itaipa nchi nafasi ya kujulikana zaidi duniani katika
sekta ya utalii.
Post a Comment