Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TANESCO YAIBIWA NGUZO ZA BILIONI 3.5/-

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba
********
Watu wanaodhaniwa kuwa wezi, wamefungua na kuiba nati za nguzo kubwa za vyuma za umeme Kahama, mali ya Shirika la Ugavi wa  Umeme Tanzania (Tanesco) na kusababisha hasara ya Sh. bilioni 3.5.
 
Taarifa iliyotolewa  kwa vyombo vya habari  juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba,  ilisema wizi  huo  ulifanyika Januari 10,  mwaka huu katika kijiji  cha  Kakola B, Kata ya  Kakola wilayani  Kahama na kusababisha usumbufu na hasara  kubwa kwa wananchi, mgodi wa dhahabu Bulyanhulu na shirika hilo.
 
Alisema mbali na hasara, hali hiyo  imesababisha miji ya Shinyanga, mgodi wa  Bulyanhulu pamoja na mji wa Kahama  kukosa huduma ya maji kwa muda wa wiki mbili.
 
Kwa mujibu wa Mramba, nguzo zilizofanyiwa hujuma zimo katika njia kubwa ya umeme wa Kilowati 220.
 
Mramba  ambaye  alitembelea  eneo la tukio ili  kujionea shughuli za ujenzi unaoendelea,  alisema wizi huo utaisababishia shirika hasara  ya  Sh. bilioni 3.5  ili  kurejesha  nguzo hizo.
 
Alisema nguzo iliyofanyiwa hujuma kubwa ni namba 266  na baada ya kuanguka ilisababisha  nguzo jirani, namba 277 pia kuanguka na kusababisha kukosekana kwa umeme kwa wateja wanaotegemea laini hiyo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top