Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

USHAURI WA KINANA NA NAPE DHIDI YA MAAMUZI YA RAIS KIKWETE KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI

 



Nape  kushoto akiwa na Kinana


 Mwenyekiti  wa CCM  Rais Kikwete
 
............................................
Na Francis Godwin Blog
MATEGEMEO yangu binafsi  bila  shaka  ni mategemeo ya watanzania  wengi  wapenda maende maendeleo wakiwemo hata  wana chama wa  chama chao cha  CCM na vyama vya upinzani  kikiwemo Chadema  ambao  nilipata  kumsikia katibu mkuu  wake Dr  Slaa akiunga mkono kauli ya katibu  mkuu wa CCM Bw  Kinana japo kwa mtazamo tofauti kwa  kutaka aliyewateuwa  mawaziri mizigo pia ajiuzulu .

Yawezekana  kabisa  wengi  wetu  tulitegemea  ucheleweshaji wa uteuzi wa mawaziri  wanne  waliotenguliwa nafasi zao na yule waziri wetu  wa fedha  Dr Wiliam Mgimwa  aliyefariki  dunia ni kutokana na Rais  wetu Jakaya Kikwete  kuangalia  wabunge wenye  sifa  watakaoziba nafasi za hao  waliotenguliwa uteuzi  wao na wale  watakao shika nafasi  za mawaziri  waliotajwa na chama  kuwa ni mizigo  .
Kwani  sikutegemea  kuona mwenyekiti  wa CCM Taifa  Dr  Kikwete akipuuza  kirahisi  zaidi  maoni ya  katibu  wake mkuu na katibu  wake wa itikadi na uenezi Bw Nape  Nnauye  ambao wamepata  kuzunguka maeneo  mbali mbali ya Tanzania  na  kupokea maoni ya  watanzania  juu ya utendaji kazi  wa waziri mmoja  baada ya mwingine na serikali kwa ujumla na hata  kufikia hatua ya  kutumia majukwaa ya siasa  ya  CCM kuwataja kwa majina  waziri  mmoja hadi mwingine  jinsi gani walivyokuwa mzigo  katika baraza la mawaziri.

Wengi wetu  tulipokea  kwa mikono miwili utendaji kazi wa katibu Kinana na Nape  na hata  kupongezwa  kwa  kuliona  hilo na huku  tukisubiri nyufa  hiyo  iliyojitokeza  kuona inazibwa vema na mwenyekiti  wa baraza la mawaziri rais Kikwete ambae  ndie  aliwateua kumbe  sio tulivyotegemea.

Ikumbukwe  mawaziri waliotajwa  kuwa ni mizigo ni pamoja na   Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza na Naibu wake, Adam Malima kuwa  wameshindwa kazi na kupendekeza wang’olewe.

Kauli hiyo ambayo ilitolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, akisema kuwa mawaziri hao wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia Watanzania.

Alisema anasikitishwa na kitendo cha mawaziri hao waliopewa dhamana kushindwa kutambua wajibu wao na kwamba umefika wakati wa kuhojiwa na Kamati Kuu (CC) ya CCM ili wachukuliwe hatua kwani bila kufanya hivyo aibu itarudi kwa chama chake.

Nape alitoa kauli hiyo kwa nyakati  tofauti  katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wakati akielezea changamoto zinazowakabili wakulima ambao ni asilimia 80 ya Watanzania, huku mawaziri husika wakikaa kimya.

Alisema kuwa Waziri Chiza na Malima wamebaki wakifunga tai na kuvaa suti mjini wakati wakulima wa Ruvuma na mikoa mingine ya Tanzania wakiteseka.

Nape alisema Waziri Kawambwa naye anatakiwa kuchukuliwa hatua kwa kuingia mkataba na kampuni ya ujenzi ya Progressive iliyopewa zabuni ya kutengeza barabara ya Natumbo hadi Tunduru wakati mkandarasi huyo hana uwezo wa kuijenga na matokeo yake amefukuzwa kazi.

Dk. Kawambwa ametupiwa lawama hizo kutokana na kuipa kazi kampuni hiyo wakati akiwa Waziri wa Miundombinu pamoja na kushindwa kusimamia elimu.

Akiwazungumzia Chiza na Malima, Nape alisema inasikitisha kuona wakulima wakiteseka, lakini waliopewa dhamana ya kuwasaidia wakishindwa kuwasikiliza na kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao.

“Nitahakikisha mawaziri hao wanachukuliwa hatua ikiwa pamoja na kuwajibishwa na chama na ikishindikana tutatumia wabunge wetu kufanya kazi hiyo,” alisema Nape ambaye anaongozana na, Kinana, katika ziara ya kichama kwenye mikoa ya Kusini na Nyanda za Juu Kusini.

Nape alisema akiwa katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kila eneo wananchi wanawalalamikia Chiza na Malima kwa mambo mbalimbali hivyo suala hilo linapaswa kufikia mwisho wake maana chama hakiwezi kuwavumilia.

“Katibu Mkuu (Kinana), nilimuuliza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Chiza na Malima wamefika lini kusikiliza matatizo ya wakulima wa tumbaku, korosho na mahindi, alinijibu hakumbuki kama wamefika mkoani hapa. Nikafuatilia na kubaini si yeye tu hata Waziri aliyetangulia Profesa Jumanne Maghembe naye hakuwahi kufika. Najiuliza sababu nini, hakuna majibu,” alisema Nape.

Nape alisisitiza kuwa yuko tayari kupoteza nafasi aliyonayo kuliko kuacha Watanzania wakiendelea kuteseka kwa ajili ya mawaziri wachache waliopewa dhamana na Serikali ambayo ni ya CCM, lakini hawatimizi wajibu wao.

“Kwa hili hata chama changu na Katibu Mkuu mkiamua kunifukuza nipo tayari, ni bora nikawe mkulima, lakini kwa kuwa nafanya kazi ya kuwatetea wananchi watanilinda tu,” alisisitiza Nape.

Alitumia nafasi hiyo kumuomba Kinana apeleke ripoti ya mawaziri hao kwa CC wachukuliwe hatua na ikiwezekana waitwe wahojiwe.

Nape aliongeza: “Wananchi naomba mnilinde, lakini niseme ukweli. Mawaziri ambao tumewapeleka jikoni wameshindwa kupika chakula, tunasubiri sebuleni, lakini chakula hakiji. Wanatukwamisha, ni bora wakaondoka kama wameshindwa kazi.”

“Mimi ni kijana, sipo tayari kuona CCM inakuwa chama cha upinzani bungeni kwa sababu tu ya hawa wenzetu wachache ambao wanafanya makusudi na uzembe katika kutekeleza wajibu wao.

Kuhusu barabara ya kutoka Songea hadi Namtumbo, alisema anamshukuru Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kwa kumfukuza mkandarasi huyo, lakini

hiyo pekee haitoshi wale wote waliohusika kumpa mkataba wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa kuwa Serikali imepata hasara.

“Dk. Kawambwa amekuwa akitukwamisha CCM katika kutimiza wajibu wake. Hii barabara ya Namtumbo hadi Tunduru kushindwa kukamilika imeleta aibu kubwa na kututia fedheha. Hivyo lazima waliotoa mkataba wawajibishwe,” alisema Nape.

Kwa mujibu wa Nape, Dk. Kawambwa pia ameshindwa kushughulikia matatizo ya walimu nchini na kumkumbusha kuwa alipewa muda wa miezi sita na CCM na inakaribia kumalizika. Hata hivyo, hakufafanua miezi sita aliyopewa Waziri Kawambwa inahusu nini.

“Muda ukimalizika tutataka kufahamu yale ambayo tumeyaagiza kama yamefanikiwa na iwapo atakuwa ameshindwa ajue hatutakaa kimya,” alisema
Nape.

Alifafanua kuwa yeye (Nape) kama msemaji wa CCM kamwe hatakaa kimmya wakati chama kikipata aibu kwa kutotekelezwa miradi mbalimbali iliyoahidiwa katika Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010.

Naye Katibu Mkuu Kinana alisema katika kikao cha CC kitakachofanyika mwezi ujao, kitamuandikia barua Rais Jakaya Kikwete ili mawaziri wake waende mbele ya kikao na kueleza kwa nini wasifukuzwe kwa kushindwa kazi.

Alisema kuwa haiwekani kuwa na Serikali ya walalamikaji kwa mfano mkuu wilaya analalamika, mbunge analalamika na kuweka wazi kuwa ni lazima yafanyika maamuzi magumu.

“Kama hali ndiyo iko hivi je, mwananchi wa kawaida atakwenda wapi. Hili sasa limefika mwisho, ni lazima wenzetu waliopewa dhamana wawajibike,” alisema Kinana.

Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wa CCM kuwataja kwa majina mawaziri hadharani kueleza wazi kuwa wamshindwa kutimiza wajibu wao na kuwataka wang’oke madarakani.

Kadhalika, ni mara ya kwanza kwa Katibu Mkuu wa chama tawala kuinga mkono kutajwa kwa majina ya mawaziri hadharani na kueleza wazi kuwa watawashitaki kwenye chama na kuwataka wajieleze mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho.

Sasa  tujiulize kama Rais  Kikwete katika uteuzi huu ameshindwa  kuchukua hatua na hata  kuwapandisha  vyeo mawaziri  hao  mizigo na kutoa kafara kwa naibu   wa elimu na mafunzo ya mafunzo Philip Mulugu na  kumuacha  aliyetajwa  boss wake Kawambwa ni  kusema ushauri  wa akina  Kinana na Nape  umepuzwa ambao ni ushauri  wa Chama  cha  CCM .

Ila  mbaya  zaidi mbali ya  kushindwa  kuwawajibisha   mawaziri hao mizigo  bado  walioteuliwa ni  heri hata  ya  waliokuwepo  sasa katika uteuzi huu kwa lugha nyepesi  ni kusema tumeruka majivu na kukanyaga moto nini hatima yake.

Pia  tujiulize  hawa  walkioteuliwa ni kwa ajili ya nani  ni kwa faida ya  watanzania amao kuna  jambo lipo nyuma ya pazia kweli  kama  mimi ningetakiwa  kutoa ushauri wa baraza  basi lazima ningeanza na wale  waliotajwana chama kuwa ni mizigo kwa kuwaondoa kabla ya kuwaondoa  waliokwisha  jiondoa akina Kagasheki na  wenzake .

Ila  pia ushauri  wangu  kwa Kinana na Nape ni vema kabla ya  kuanza  kukata  tawi  kuangalia wapi  linaangukia na litachukuliwa baada ya  kuanguka ama litasimamishwa  tena kwani ninachoona hata akina Kinana na  Nape wamepuuzwa na yawezekana  wanaonekana kuwa na chuki  binafsi na waliowataja kuwa ni mizigo  wakati yeye ameona  si mizigo na kama Kinana na Nape  kweli  wanaipenda  kazi hiyo ni vema kwa heshima ya  chama kujiuzulu  badala ya  kuendelea  kupokea fedheha na hata  wakirudi katika mikoa waliozunguka  kutoka kauli ya kuwapinga mawaziri hao  yawezekana  wakajishushia  heshima yao .

Ushauri  wangu kwa Kinana na Nape kabla ya  kutoa kauli nzito kama hizo  kuuliza misimamo ya  viongozi wenu wa juu badala ya  kugeuka kuwa ni  wavurugaji katika serikali na chama chenu na kama mnaona utafiti  wenu wa kuwa hao ni mawaziri mizigo ni wa

kweli basi chukueni  hatua ya  kujiuzulu maana aliyewateua  hajaona kuwa ni mizigo na hata  kuwapuuza  basi  mjue heshima yenu  imeshuka maana mtaonekana ninyi ni watu wa majungu.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top