Waziri
wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akimsikiliza Baloziwa Norway
(kushoto), Bi. Ingunn Klepsvik pamoja na maafisa wake na kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa DAWASA, Archad Mutalemwa.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na Balozi wa Norway, Bi. Ingunn Klepsvik.
Balozi wa Norway, Bi. Ingunn Klepsvik, jana alitembelea Wizara ya Maji na kuonana na Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe.Balozi
huyo alipata fursa ya kuzungumza na Prof. Maghembe kuhusu hali halisi
ya sekta ya maji nchini na miradi mbalimbali ambayo Serikali ya Norway
inafadhili.Bi.
Klepsvik aliambatana na maafisa mbalimbali kutoka ubalozi wa Norway,
huku Wizara ya Maji ikiwakilishwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,
Inj. Bashir Mrindoko, Kaimu Mkurugenzi wa Maji Mijini, Inj. Amani Mafuru
na Mkurugenzi Mtendaji wa DAWASA, Archad Mutalemwa.
Mkurugenzi
na Mtendaji Mkuu wa GAiN, William Blaney (katikati) akizungumza,
walipomtembelea Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (hayupo pichani),
kulia ni wenzake walioongoza nao na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko.Ugeni
kutoka Kampuni ya Global Aid Network (GAiN) jana ulimtembelea Waziri wa
Maji, Prof. Jumanne Maghembe na kuzungumza nae kuhusu utendaji wao wa
kazi na mafanikio yao katika kusaidia kukuza sekta ya maji hapa nchini. Kampuni
hiyo ya Canada inayoongozwa na William Blaney inahusika na uchimbaji
visima vya maji barani Afrika katika nchi za Togo, Benin, Ethiopia,
Sudan ya Kusini na Tanzania. Mpaka sasa imeweza kutekeleza uchimbaji wa visima 222 mkoani Lindina 122 kati ya hivyo vikiwa vinatoa huduma ya maji.
Post a Comment