Magari yakipishana kwa shida katika eneo hilo la Kijiji cha Mkalapa,Mkoani Mtwara kutokana na kuharibika kwa barabara hiyo.
Wakazi wa
kijiji hicho pamoja na Abiria wanaosafiri kwenda
Newala,Masasi,Nachingwea,Nanyumbu na Tunduru wakiwa wamesimama bila
kujua cha kufanya wakati magari yakiwa yamekwama.
*******
*******
Na Abdulaziz ,Masasi.
Barabara
ya Ndanda kwenda Masasi eneo la Kijiji cha Mkalapa,limekuwa ni majanga
matupu kama inavyoonekana katika picha hapo chini,kwani barabara hiyo
imeharibika vibara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha matika maeneo
mbali mbali hapa nchini.
Abiria
wanaofanya safari katika maeneo hayo,inapaswa wajiandae kwa kupoteza
masaa kadhaa katika eneo hilo,kwani mambo hayajakaa sawa.
Hivyo
wakala wa Barabara Mkoa wa Mtwara (TANROADS),wanapaswa kulishughulikia
swala hili haraka iwezekanavyo ili kuwaepusha watumiaji wa barabara hiyo
kuondokana na hadha hii inayowaathiri wasafiri waendao
Newala,Masasi,Nachingwea,Nanyumbu na Tunduru.
NA MTWARA YETU
Post a Comment