Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Kanda ya Ziwa Mashariki leo kimewavua nyadhifa zao viongozi wake watano wa jimbo la Kahama kwa makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukiuka taratibu za chama hicho.
Uamuzi huo umetolewa na
Mratibu wa Chedema Kanda ya Ziwa Mashariki Renatus Nzemo katika kikao
kilichofanyika katika ofisi ya Kanda ya Ziwa Mashariki na kupitia mazimio hayo
kabla ya kutoa uamuzi.
Viongozi waliovuliwa nyadhfa
zao ni Mwenyekiti wa jimbo la Kahama Israel Barikiel, Katibu wa Jimbo Vicent Kilukilwa,
Katibu Mwenezi wa jimbo Bobson Wambura, Mwenyekiti Bawacha Kasigwa Adram na
Mwenyekiti Bavicha Benedict Shija.
Katika Barua yake aliyoiandika
kwa viongozi hao, Nzemo amesema viongozi hao wanakabiliwa na tuhuma za kikiuka
tamko la kamati kuu ya chama lililowazuaia wanachama wote kushirikiana na
aliyekuwa naibu katika mkuu wa chama hiccho Zitto Kabwe.
Tuhuma zingine ni kushiriki
kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya Ubagwe kupitia chama cha TADEA, huku
viongozi hao wakipita na kujinadi kuwa wako tayari kumfuata Zitto popote
atakapokuwa.
Aidha Nzemo amesema viongozi
hao wamekuwa wakitumia nembo ya CHADEMA kunadi chama kingine cha Alliance for
change and Transparency (ACT), kinyume cha maadili ya CHADEMA katika katiba
yake ya mwaka 2006.
Nzemo amesema kutokana na tuhuma
hizo na zile zilizotolewa na baraza la mashauriano wilaya ya Kahama, viongozi
hao wanatakiwa kukabidha ofisi na vifaa vya chama kwa baraza la wazee jimbo la
Kahama mara wapatapo barua hizo.
..Via Dunia kiganjani blog
..Via Dunia kiganjani blog
Post a Comment