Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WANANCHI WAUA WATU WAWILI KWA TUHUMA YA WIZI,TUNAOMBA RADHI KWA PICHA ZINAZOTISHA


Miili ya marehemu hao baada ya kupakizwa katika gari la polisi wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga
Gari la polisi wilaya ya Kahama likiwa limezungukwa na wananchi eneo la tukio
 
Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni wezi wameuawa kwa kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi kwa kisingizio cha kuwa na hasira kali katika mtaa wa Mayila kata ya Nyihogo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Tukio hilo la mauaji limetokea leo majira ya saa tisa alasiri baada ya vijana hao kuhisiwa kuhusika na matukio ya wizi ambayo yamekuwa yakitokea katika eneo hilo mara kwa mara na kuwakosesha amani wananchi.

Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Nyihogo Amos Sipemba, aliyefika eneo la tukio mara baada ya mauwaji hayo, amesema hadi sasa mmoja wa marehemu ametambulika kwa jina la Joseph Bakuku huku mwingine akiwa bado hajafahamika.

Sipemba amesema huenda kufanyika kwa mauaji hayo kunatokana na wananchi hao kuwahisi vijana hao kuhusika katika matukio mawili ya uvamizi yaliyotokea usiku wa kuamkia jana katika kata hiyo na kuripotiwa ofisini kwake.

Jeshi la Polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba miili ya marehemu hao imehifadhiwa katia chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Wilaya ya Kahama, huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.
Credit-Dunia kiganjani
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright 2025 EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG | Designed By Code Nirvana
Back To Top