Mkakati wa kumuingiza Chenge katika Bunge hilo unadaiwa kuwa na lengo la kuhakikisha anasimamia vilivyo hoja na msimamo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutaka muundo wa serikali mbili ulioboreshwa.
Ingawa kazi ya uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi hiyo inayomezewa mate na baadhi ya viogogo wa CCM, yakiwemo makundi ya urais mwaka 2015, jina la Chenge linaonekana kung’ara na limekuwa likipigiwa chapuo na makada wazito wa chama hicho tawala.
Post a Comment