 |
Hayati Nelson Mandela, aliachia familia yake mali yake yenye thamani ya dola milioni 4.1.
Sehemu ya mali hiyo pia itatolewa kwa chama tawala ANC, wafanyakazi wake wa zamani na shule kadhaa ambako alisomea.
Hayo ndio yalikuwa mapenzi ya Mandela ambayo yalikuwa kwenye wasia wake uliosomwa hadharani kwa familia nzima.
Afisaa
Dikgang Moseneke aliyekabidhiwa jukumu la kusoma wasia huo wenye kurasa
40 na kuhakikisha unatekelezwa ,alisema hapajakuwa na pingamizi zozote
kuhusu yaliyomo kutoka kwa familia ya Mandela.
Wafanyakazi
wa karibu wa Mandela watapata randi 50,000 kila mmoja. Shule ambazo
Mandela alisomea zitapata randi laki moja kila shule.
Hayati Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95.
Familia
ya Mandela tangu hapo imekuwa ikizozana kuhusu urithi wa hayati Mandela
na kuna hofu kuwa huenda wasia huu ukasababisha mgogoro mwingine kuhusu
mali hiyo.
Mali
ya hayati Mandela inajumuisha nyumba na hakimiliki za vitabu ikiwemo
kimoja kuhusu maisha yake kwa jina ''Long walk to freedom''
|
on Monday, February 3, 2014
Post a Comment