Mshambuliaji
wa klabu ya Arsenal Olivier Giroud ameomba msamaha hadharani kupitia
mtandao wa kijamii wa Twitter kufuatia kugundulika kwa usaliti kwenye
ndoa yake.
Kwa takribani wiki moja sasa hivi kumekuwa na tetesi kwamba Mfaransa
huya alimsaliti mkewe kwa kutoka na mwanamitindo Celia Kay likiwa ni
tukio lililotokea usiku wa kuamkia mechi ya Arsenal vs Crystal Palace
February 2 2014 hotelini London.

Gazeti la Sunday Sun lilikuwa la kwanza kuripoti taarifa hizo lakini Giroud alisema ni uongo, lakini jana gazeti hilo likatoa ushahidi wa picha ambayo inasemekana ilipigwa na Kay, ikiwa inamuonyesha Giroud akiwa kavaa nguo ya ndani wakiwa bado chumbani.

huyu wa kifaransa ambaye alikanusha taarifa hizo mwanzoni, hakuwa na
jinsi tena zaidi ya kukiri kutokea kwa tukio hilo na kuamua kuomba radhi
kupitia page yake ya twitter.
Post a Comment