Jeshi
la Polisi nchini, linapenda kuufahamisha umma kuwa, mnamo tarehe
15/02/2014 siku ya Jumamosi katika viwanja vya Polisi Barracks, barabara
ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, kutakuwa na hafla ya kumuaga IGP
Mstaafu Said Alli Mwema kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana.
Katika hafla hiyo, kutakuwa na mambo mbalimbali yaliyoandaliwa ikiwemo gwaride maalum la heshima.
Ikumbukwe
kuwa, katika kipidi chake cha uongozi wa Jeshi la Polisi, IGP Mstaafu
Said Alli Mwema alishirikiana vyema na wananchi wa kada zote wakiwemo
wadau mbalimbali wa amani, hususani katika dhana ya Ulinzi shirikishi na
Polisi Jamii. Jeshi la Polisi nchini kwa kulitambua hilo, linatumia
fursa hiyo kuwakaribisha wananchi wote kuhudhulia hafla hiyo.
Aidha,
IGP Mstaafu Said Alli Mwema katika uongozi wake alianzisha na kusimamia
mifumo mbalimbali ya kuzuia na kukabiliana na uhalifu hapa nchini
ikiwemo maboresho ndani ya Jeshi la Polisi, ili kuhakikisha Jeshi
linafanya kazi kwa weledi, usasa na ushirikiano na wananchi.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Post a Comment