JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 08 WOTE RAIA NA WAKAZI WA
SANGE – BUKAVU NCHINI KONGO WAKIONGOZWA NA HESABU LUHIGITA (16) BAADA YA
KUINGIA NCHINI BILA KIBALI. WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE
12.02.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA IKUMBILO
WILAYA YA ILEJE WAKIWA WANASAFIRISHWA KWENYE GARI LENYE NAMBA ZA
USAJILI T.136 AQC AINA YA FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA MUSSA DISI
(35) NA MATEO KADUMA (30) WOTE WAKAZI WA ISONGOLE AMBAO PIA WAMEKAMATWA
PAMOJA NA GARI HILO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA
KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI KUHUSIANA NA MTU/WATU WANAOWATILIA
SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO
ZICHUKULIWE.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment