Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na
Mazingira Mhe. Abdulkarim Shah akiwasili kwa boti katika Hifadhi ya
Taifa ya Gombe, Kigoma.
Mkurugenzi
Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi akiwakaribisha Wajumbe wa Kamati
ya Ardhi, Maliasili na Mazingira katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe
Bibi. Noelia Myonga, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmoud
Mgimwa,Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Abdulkarim Shah na Mkuu wa
Wilaya ya Uvinza Bibi. Hadija Nyembo.
Katikati
ya Msitu wa Gombe Wajumbe wa Kamati wakipumzika kwa muda wakiwa njiani
kuelekea katika Maporomoko ya Maji ya Kakombe huku wakimsikiliza Mkuu wa
Hifadhi Bibi Noelia Myonga (kushoto).
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Abdulkarim Shah akiwaongoza wenzake kuelekea
katika Maporomoko ya Maji ya Kakombe katika Hifadhi ya Gombe.
Wajumbe wa Kamati wakiwa katika picha na baadhi ya watumishi katika Maporomoko ya Maji ya Kakombe.
Baadhi
ya watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe wakimsikiliza Makamu
Mwenyekiti wa Kamati wakati wa kuagana mara baada ya kumaliza ziara yao
hifadhini.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe.
Abdulkarim Shah (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari
ya Kagongo wilayani Kigoma madarasa manne yaliyojengwa na Hifadhi za
Taifa kupitia Hifadhi ya Gombe.
Madarasa manne katika Shule ya Sekondari ya Kagongo wilayani Kigoma yaliyojengwa na Hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Post a Comment