Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kamati ya Kumshauri Mwenyekiti wa muda wa Bunge Maalum yawasilisha taarifa

prof-mahalu-top


  NA MAGRETH KINABO- MAELEZO,DODOMA

Kamati  ya  Kumshauri  Mwenyekiti wa muda wa Bunge Maalumkuhusu Kanuni za Bunge Maalum  leo imewasilisha taarifa katika  semina  iliyoandaliwa kwa wajumbe wa bunge hilo ,ambapo imependekezwa mambo mbalimbali, likiwemo  kuwepo kwa Siwa na wagombea  uenyekiti na makamu mwenyekiti  kutojitoa katika nafasi zao baada ya uteuzi wa wagombea.
 Akiwasilisha taarifa hiyo Mwenyekiti wa kamati hiyo,Profesa Costa Mahalu  wakati wa semina kuhusu kaununi hizo kwa  wabunge hao , alisema kamati Mwenyekiti huyo alisema  kuwepo kwa Siwa  Mahsusi  ambalo baada ya bunge hilo kukamilisha shughuli zake litatunzwa kama kilelelezo cha kumbukumbu ya tukio hilo muhimu la kihistoria.
Alizitaja namna Siwa hilo litakavyokuwa ni urefu wa mita 1.2,uzito wa 4.5kgs, madini ya dhahabu na aluminium na muonekano wenye alama mbalimbali , ambazo ni kitabu, michoro ya watu wa makundi mbalimbali walioshiriki kutunga Katiba ya Tanzania kwa mujibu wa sheria, rangi, nembo  na bendera ya taifa na kalamu unnaounganisha kichwa na mkonga.

 Profesa Mahalu aliongeza kuwa kamati hiyo imependekeza kuwepo kwa Siwa mbili ili moja iwekwe kama kumbukumbu kwa uapande wa Tanzania Bara na nyingine Zanzibar.
 Alisema kamati  hiyo imeongeza kanuni za uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum, ambapo imeweka fomu  ya mgombea wa nafasi hizo na karatasi ya kupiga kura.
Mambo mengine yaliyopendekezwa katika rasimu hiyo ni  watu wenye mahitaji maalum kuruhusiwa kutumia vifaa maalum ili waweze waweze kuonekana kwa urahisi kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum na kupewa nafasi ya kusema wakiwa katika  ukumbi wa mikutano ya bunge hilo na wasaidizi wa wajumbe wenye wenye mahitaji maalum waruhusiwe kuingia katika ukumbi huo ili wawasaidie wajumbe hao katika zoezi la kupiga kura na kupata usaidizi mwingine watakouhitaji ukumbini.
 Aidha alisema kamati hiyo imependekeza wakati Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba anapowasilisha Rasimu ya Katiba wajumbe wasiruhusiwe kuomba ufafanuzi, utaratibu au mwongozo wa Mwenyekiti.
Aliongeza kuwa kamati hiyo imependekeza kuwa katika uendeshaji wa shughuli za Bunge Maalum pale ambapo mjumbe hataridhika na uamuzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum kuhusu sula linalohusu Kanuni za Bunge Maalum, mjumbe huyo akate rufaa kwa Kamati ya Kanuni na Haki za  Bunge, ambayo Mwenyekiti anayekatiwa rufaa hatakalia kiti,na pia rufani hiyo ifanyiwe kazi na taarifa yake itolewe katika bunge hilo ndani ya kipindi kisichozidi siku tano.

Pia imependekeza ili vikao wa bunge hilo vianze  idadi ya wajumbe wa bunge hilo iwe nusu kwa nusu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, ambapo awali ilikuwa ni nusu ya wajumbe wote.
Katika taarifa hiyo imependekezwa kuwa viongozi wa bunge hilo kwa kufuata misingi ya haki na bila upendeleo wowote wasiruhusiwe kuhudhuria vikao vyoyote ambavyo vinajadili na kuweka msimamo juu ya suala lolote linalojadiliwa au litakalojadiliwa na bunge hilo.  
 Profesa Mahalu alisema kamati hiyo inapendekeza kanuni mpya inayohusu Rais wa Jamhuri ya Muungano, Rais wa Zanzibar  au Rais wa nchi nyingine kutambuliwa kama wageni rasmi wanaoweza kualikwa na Mwenyekiti wa bunge hilo na kulihutubia.
Aidha  alifafanua kwamba kamati hiyo inapendekeza kuainisha mavazi rasmi yanayoruhusiwa katika bunge hilo.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top