NA MAGRETH KINABO – MAELEZO DODOMA
Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba ,Pandu Ameir Kificho Aidha Mwenyekiti huyo amevitaka vyombo vya habari kuandika habari za bunge hilo kwa kupata ufafauzi sahihi kutoka mamlaka husika.
Aidha Mwenyekiti huyo ametoa ufafanuzi wa kuahirishwa kwa vikao vya bunge hilo katika kipindi cha wikii hii kumetokana na kutokamilishwa kwa kwa Kanuni za Bunge Maalum la Katiba.
“ Uahirishaji wa vikao vya Bunge Maalum la Katiba ulikuwa ni wa kutoa nafasi kwa wabunge kujisomea kanuni hizo kwa makini na kupata ushauri,” alisema Kificho.
Aliongeza kuwa bila ya kupata msingi wa kanuni za bunge hilo , itakuwa rahisi kujadili Rasimu ya Katiba kama walivyotumwa na Watanzania.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma baada ya mmoja wajumbewa bunge hilo, Richard Ndassa kuomba mwongozo kufutia baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kuwa “wabunge wachota milioni 150 kwa dakika 25 na “Bunge la Katiba vipande vipande wapewa posho kwa kusoma magazeti”.
“ Kazi ya kanuni haijakamilika, hatuwezi kuendesha Bunge bila kanuni jamani huu ndio uandishi naomba mwongozo wako,” alisema Ndassa.
Akifafanua kuhusu suala hilo Kificho alisema aliwahi kuzungumza na vyombo vya habari(ITV na Radio One kuhusu jambo hilo, hivyo si vema vyombo vya habari kuandika bila ya kupata ufafanuzi kutoka mamlaka husika.
Aliongeza kuwa masuala yote yanayoendelea katika bunge hilo yanakwenda kwa mujibu wa sheria.

Post a Comment