Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Hajjat Amina Mrisho Said akizungumza na
Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa watu wenye Uwezo wa
Kufanya Kazi kutoka mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na
Mtwara walio katika mafunzo ya siku 16 leo mjini Morogoro. Kulia Bw.
Mhidini Mtindo, Mtakwimu Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

Wadadisi
na Wahariri wa madodoso ya watu wenye uwezo wa kufanya Kazi kutoka
mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara wakiwa kwenye
mafunzo ya siku mjini Morogoro. 
Kamishna
wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Hajjat Amina Mrisho Said akiwa katika
picha ya pamoja na Wadadisi na Wahariri kutoka mikoa ya Dar es salaam,
Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara walio katika mafunzo ya siku 16 leo
mjini Morogoro.
……………………………………………………………………..
Na. Veronica Kazimoto na Aron Msigwa – Morogoro.
Na. Veronica Kazimoto na Aron Msigwa – Morogoro.
Wadadisi
na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi
mwaka 2014 wametakiwa kuzingatia maadili na weledi katika utekelezaji
wa majukumu yao ili kuepuka kuliletea taifa hasara kwa kutoa takwimu
zisizosahihi.
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini Morogoro na Kamishna wa Sensa ya Watu na
Makazi Bi. Hajjat Amina Mrisho Said wakati akizungumza na Wadadisi na
Wahariri wa madodoso yaUtafiti wa Watu wenye uwezo wa kufanya kazi
kutoka mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara walio
katika mafunzo ya siku 16 mjini Morogoro.
Amesema
ili majibu ya takwimu zinazokusanywa yawe sahihi ni lazima wataalam
hao wazingatie kanuni na taratibu zilizowekwa katika kupata uhalisia wa
taarifa za watu za eneo husika badala ya kutoa takwimu zisizo sahihi.
“Tunachotegemea
kutoka kwenu ni kwamba mtakayojifunza na kuyafanya kwa vitendo hapa
mtakwenda kuyafanyia kazi na kutuletea takwimu sahihi na sio za kupika
mtaani, na kuepuka kuzungumza na watu wachache wa kikundi Fulani
kuwakilisha maeneo yote” Amesisitiza.
Amesema
kuwa yapo mambo mengi ya kuzingatia ambayo wao kama wadadidisi na
wahariri wanapaswa kuyafuatilia wakati wa ukusanyaji wa takwimu hizo
ikiwemo idadi ya watu wenye umri wa kwenda shule ambao bado wako
nyumbani ili kuisaidia serikali kupanga mipango ya maendeleo.
Ameongeza
kuwa ukusanyaji wa takwimu hizo ni muhimu kwa sababu zinaondoa utata
katika kushughulikia changamoto mbalimbali katika maeneo mbalimbali
ikiwemo uwepo wa usahihi wa taarifa kuhusu makundi ya watu na kazi zao,
kipato,masomo, uwezo wa kufanya kazi na utegemezi na kuondoa tatizo la
baadhi ya taasisi kutumia takwimu zisizo sahihi kujipatia fedha isivyo
halali kwa mambo yasiyokuwepo.
Akitoa
ufafanuzi wa takwimu zilizopo nchini kutokana na matokeo ya Sensa ya
Watu na Makazi ya mwaka 2012 Bi. Hajjat amesema kuwa kiwango cha
ongezeko la idadi ya watu kutoka sensa ya mwaka 2002 mpaka 2012 ni
asilimia 2.7 kwa maana ya ongezeko la watu milioni 10 ndani ya miaka 10
na kufafanua kuwa ni sawa na ongezeko la watu milioni 1 kila mwaka ni
kubwa ikilinganishwa na hali ya uchumi uliopo.
Kuhusu
mikoa ambayo wawakilishi wake wako katika mafuzo amesema kuwa mkoa wa
Morogoro idadi ya watu imeongezeka kwa asilimia 2.4, mkoa wa Pwani
asilimia 2.2, Dar es salaam 5.6 ongezeko ambalo ni kubwa sana.
“Hii
ni changamoto kubwa sana kwa mkoa wa Dar es salaam na ipo haja ya
kuchukua hatua kwa sababu kila kilometa moja ya mraba wanaishi watu 3133
hata sehemu ya kumwaga taka na sehemu ya kupitisha maji inakuwa tatizo
kutokana na msongamano wa watu’’ amesisitiza.
Aidha
katika mkoa wa mkoa wa Lindi idadi ya watu imeongezeka kwa asilimia
0.9, Mtwara ikifikia asilimia 1.2 na kuongeza kuwa kuna uwezekano mkubwa
wa idadi hiyo kuongezeka zaidi kutokana na ugunduzi wa gesi na mafuta
katika mkoa wa Mtwara ongezeko la watu katika mkoa huo litakuwa kubwa
kutokana na uwekezaji mkubwa katika mkoa huo.


Post a Comment