Katibu
Tawala Mkoa wa Katavi Injinia Emmanuel Karobelo Katibu Mkuu wizara ya
maendeleo ustawi wa Jamii mama Anna Maembe wakati akikagua eneo la chuo
cha maendeleo Msaginya wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo
anaye mfuatia kushoto kwa Katibu Mkuu ni Afisa Maendeleo ya Jamii
Halmashauri ya Wilaya Nsimbo Alex Magesa Na Mwisho mwenye SUTI YA kijivu
ni Mkuu wa Chuo Msaginya Peter Kikunda ambaye ni mwenyeji akiwatembeza
wageni.
………………………………………………………………………………….
Na Kibada Ernest- Katavi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Manedeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Anna Maembe ameshauri watendaji wa Wizara hiyo kuwa wabunifu katika
utendaji wao wa kazi za kila siku kwenye maeneo yao ili kuleta
mabadiliko katika jamii wanayoitumikia katika utendaji wao wa kazi.
Katibu Mkuu alitoa kauli hiyo
mkoani katavi alipokutembelea mkoa huo na kukutana na watendaji wa
Wizara yake na kupata nafasi ya kukitembelea Chuo cha Maendeleo ya
wananchi Msaginya kilichoko Halmashauri ya Nsimbo Wilayani Mlele ambacho
kinakabiliwa na changamoto kibao hali iliyosababisha kushindwa kusajiri
wanachuo wa kujiunga katika fani mbalmbali mwaka huu wa masomo.
Mbali ya kukitembelea Chuo hicho
pia alipata nafasi ya kukutana na vikundi vya vya kinamama waliojiunga
pamoja kw a ajili ya kupata na mikopo wanayowezeshwa na Halmashauri
kutokana na fedha za ndani ili kuwajengea uwezo akimama waweze
kuondokana na utegemezi kwa kuanzisha baiashara ndogondogo ambazo
huwasaidia kujikimu kimaisha katika familia zao kama kusomesha
watoto,matibabu na huduma nyingine za kijamii.
Pamoja na kukutana na vikundi vya
uzalishaji mali kutoka kwenye Halmashauri za Mkoa huo za Wilaya
Mpanda,Halmashauri ya Nsimbo,pamoja na ile ya Mji wa Mpanda kupokea
changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo akinamama hao, pia alipata
nafasi ya kukutana wakurugenzi wa Halmashauri hizo na wakuu wa Idara ya
Maendeleo ya Jamii pamoja na wafanyakazi wa Idara hizo akapokea
changamoto zinazowakabili katika utendaji kazi na namna ya kukabiliana
nazo.
Awali akiwa katika ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Katavi alipokea Taarifa ya Mkoa kuhusu utekelezaji wa kazi
za Idara ya Maendeleo na Ustawi wa jamii iliyotolewa na Katibu Tawala
wa Mkoa Mhandisi Emmanuel Kalobelo kwa kueleza namna Mkoa ulivyojpanga
kukabiliana na changamoto zilizopo najinsi wanavyosaidia kuwawezesha
wananachi kuondokana na umasikini hasa kupitia Halmashauri zimejipanga
kuwezesha kwa kuunda vikundi vya akinamama pamoja na vijana kuwawezesha
kujiaajili kwa kutumia rasilimali zilizoko kwenye maeneo yao.
Akiongea katika kikao hicho
Mhandisi Kalobelo alimweleza jinsi Mkoa kupitia kwenye Halmashauri
zinavyotekeleza utendaji kazi kwa kuwaunganisha wananchi ili kuwaletea
maendeleo,kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi kupitia kwenye vikundi vya
uzalishaji mali vya akina mama na Vijana kujiunga pamoja na kuwezeshwa
mikopo kupitia kwenye Halmashauri.
Akizungumzia kipimo cha utendaji
kazi kwa mtu kuwepo kwenye nafasi Fulani aliyoanayoatapimwa na kwa
ufanisi wake kuonekena katika nafasi hiyo ameleta mabadiliko gani
kutokana na uwepo wake pale ameisaidiaje jamii kutokana na uwepo katika
nafasi hiyo.
Alisisitiza kuwa itafika wakati
kujitathimini kwa kila mmoja nini amefanya kwa nafasi aliyonayo katika
kutekeleza majukumu yake, katika nafasi aliyokabidhiwa katika kuleta
mabadiliko yenye tija katika jamii.
Katibu Tawala huyo alieleza kuwa
ni muhimu kwa kila mmoja kuwa mbunifu na kusoma mazingira ya eneo
analofanyia kazi atumie rasilimali zilizopo kuweza kuwanufaisha wale
anaowatukia awe mbunifu kwa ajili ya maendeleo ya eneo lake.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashuri ya Halmashauri ya Mpanda Estominh Chang’ah
alimweleza Katibu Mkuu kuwa Halmashauri ya Mpanda iwejiwekea mikakati ya
kuwaletea wananchi maendeleo kwa kupitia makundi ya akinamama na VIjana
kwa kuwahamasisha kujiunga kwenye vikundi vya uzalishaji mali na
kuwawezesha mikopo kutoka kwenye mfuko wa maendeleo jamii kwa kutumia
fedha zilizotolewa Halamashuri.
Akizungumzia suala la kukopa
amesema menejementi ya ukopaji ya mikopo bado haijaingia ipasavyo
miongoni mwa jamii,na mtu akipewa mkopo bado urejeshwaji wake bado uko
chini, Halamashauri katika kukabiliana na changamoto hizo imejipanga na
kujiwekea mikakati mizuri kuwahamasisha wakopaji kwa kuwape elimu namna
ya kurejesha ili wengine waweze kukopa kwa kuwa fedha hizo zinatakiwa
ziwafikie wote.
Katika kukabiliana na utatuzi wa
changamoto za uhaba wa fedha Halmashauri imeingia mkataba na benki ya
TID ili iweze kuwa inakopesha wajasiliamali wilayani mpanda ili kuondoa
tatizo la ukosefu wa fedha, Mkakati mwingine ni Halmashauri kukikwezesha
kiwanda cha uzalishaji mafuta cha Mpadeco, kuweza kusaidia kupatiwa
malighafi kwa kutumia mashamba ya alizeti ili kutoa malighafi kwa ajili
kuzalisha mafuta kwenye kiwanda hicho na ili waweze kuunza mafuta badala
ya alizeti na kuongeza thamani ya mazao.
Naye Afisa maendeleo ya Jamii
Wilaya ya Mpanda Tibenderana Justini alieleza kuwa Halmashauri yake
imejitahidi sana kuwawezesha akinamama na vijana kuwapa mikopo zaidi ya
shilingi milioni 190 na wafanyakazi wa Idara hiyo wanapata msaada mkubwa
kutoka kwenye Halamshauri kuwafikia akinamama vijijini na makundi ya
vijana kuwahamasisha kujiunga katika vikundi vya uzalisjai mali.
Mbali ya shughuli hiyo elimu
imetolewa kwa wananchi kuhusiana na suala la maendeleo ujenzi wa nyumba
bora,usafi wa mazingira, uanzishaji wa vikundi vya uzalishaji
mali,vikundi vya ufugaji nyuki ,elimu inatolewa yajuu ya kuelimisha
jamii kutokana na ukatlii kwa watoto na unyanyasjai wa wanawake na
watoto,utatuzi wa migogoro katika familia kupitia maafisa ustawi wa
jamii,
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu
alikabidhi hundi kwa Halmashauri kwa ajili ya fedha za kuwakopesha akina
mama waliojiunga pamoja katika vikundi vya uzalishaji mali,kwa
Halmashauri za zamani Halmashauri ya Mpanda na Halmashauri ya Mji kila
mmoja walkabidhiwa hudi yenye thamani shilingi million 12.na Halmashauri
ya Nsimbo ilikabidhiwa hundi yenye thamani ya shilingi milioni Saba kwa
ajili ya avikundi vya akina mama na Vijana.
Kwa nyakati tofauti wakurugenzi wa
Halmashauri hizo walishukuru kwa msaada huo wa wizara ya Maendeleo
kuwapatia fedha hizo zitasaidia kuongezea na fedha za ndani kuweza
kuwakopesha wajasilimali akinamama na vijana waweze kuondokana na
umasikini kwa kuwawezesha mikopo ili kuanzisha shughuli za uzalishaji
mali.
Akiongea kwa niaba ya wakurugenzi
wenzao Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Rashid
Neneka alishukuru Katibu Mkuu kwa kuwawezesha hundi yenye thamani ya
shilingi milioni saba kwa na kusema imefika wakati mwafaka na itasaidia
kusukuma na kupunguza tatizo la fedha za kuwawezesha kuwajengea uwezo
akina mama kwenye vikundi vya uzalishaji mali kwa kuwaondolea umasikini
akahidi kuwafedha hizo zitawafikia walengwa kwa wakati kama
zilivyokusudiwa.
Post a Comment