MTU MMOJA AUAWA KWA KUNYONGWA MKOANI MBEYA.
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA MARIA MWAWANGU (56)
MKAZI WA KIJIJI CHA UPENDO ALIKUTWA NDANI YA NYUMBA YAKE AMEUAWA KWA
KUNYONGWA SHINGO BAADA YA KUBAKWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. TUKIO HILO
LILITOKEA MNAMO TAREHE 16.02.2014 MAJIRA YA USIKU NA MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA MAJIRA YA SAA 13:30HRS MCHANA
HUKO KATIKA KIJIJI CHA UPENDO WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. MAREHEMU
ALIKUWA ANAISHI PEKE YAKE KATIKA NYUMBA HIYO. CHANZO CHA MAUAJI HAYO
KINACHUNGUZWA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA
MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KWA JESHI LA POLISI ILI
WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
MAHABUSU AJINYONGA NA KUFARIKI DUNIA WILAYANI TUNDUMA.
MNAMO TAREHE 17.02.2014 MAJIRA YA SAA 06:00HRS ASUBUHI MAHABUSU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VUMI ELIAS (30)
MKAZI WA MTAA WA MAPOROMOKO TUNDUMA WILAYA YA MOMBA ALIFARIKI DUNIA
MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA BAADA YA KUJARIBU
KUJINYONGA AKIWA NDANI YA MAHABUSU KATIKA KITUO CHA POLISI TUNDUMA.
MAREHEMU ALIINGIA KATIKA CHOO CHA MAHABUSU KILICHOPO NDANI YA MAHABUSU
HIYO MAJIRA YA SAA 04:30HRS USIKU NA KUTAKA KUJINYONGA KWA
KUTUMIA TAMBALA LA KUPIGIA DEKI. MAREHEMU ALIOKOLEWA NA ASKARI WALIOKUWA
ZAMU CHUMBA ZA MASHITAKA NA KUKIMBIZWA KITUO CHA AFYA KWA MATIBABU
AKIWA KATIKA HALI MBAYA NA HAWEZI KUONGEA BAADA YA KUPATA TAARIFA KUTOKA
KWA MAHABUSU WENGINE WALIOINGIA CHOONI HUMO. AWALI MNAMO TAREHE 14.02.2014
MAREHEMU ALIKAMATWA KWA KOSA LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA NGUVU. CHANZO
KINACHUNGUZWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA KITUO HICHO CHA
AFYA.
Signed by:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment