Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini, Joyce Fisoo akizungumza na wadau wa
Filamu Tanzania waliofika ofisini kwake kuzungumza masuala yanayohusiana
na Maendeleo ya Filamu Nchini.Kualia ni Evance Stephen Meneja Masoko wa
Kampuni ya Proin Production Ltd na Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni
ya Game First Quality Tanzania Ltd, Gideon Sangana.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini, Joyce Fisoo akizungumza na wadau wa
Filamu Tanzania waliofika ofisini kwake kuzungumza masuala yanayohusiana
na tasnia ya Filamu Nchini.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Game First Quality Tanzania Ltd, Gideon Sangana
akimueleza jambo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini, Joyce Fisoo,
wakati walipotembelea ofisi za bodi hiyo kuzungumza juu ya mambo
yanayohusiana na Maendeleo ya Filamu.
Afisa
Masoko wa Kampuni ya Game First Quality Tanzania Ltd, Moses Lupindo
akiwasilisha hoja zake kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini,
Joyce Fisoo, wakati walipotembelea ofisi za bodi hiyo.Kushoto ni Evance
Stephen Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Production Ltd, Meneja wa
Mambo ya Sheria na Ushirikiano wa Kampuni ya Proin Production Ltd, Gift
Msuya na Mkaguzi wa Filami sehemu ya Usambazaji Wil-had Tairo.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Proin Production Ltd, Evance Stephen akieleza
jambo kwenye kikao cha kujadili Maendeleo ya tasnia ya Filamu nchini,
kilichofanyika kwenye ofisi za Bodi ya Filamu Nchini
Meneja
wa Mambo ya Sheria na Ushirikiano wa Kampuni ya Proin Production Ltd,
Gift Msuya akitoa mchango wake kwenye kikao cha kujadili Maendeleo ya
Tasnia ya Filamu nchini, kilichofanyika kwenye ofisi za Bodi ya Filamu
Nchini.
Picha zote na Hussein Makame, MAELEZO
Post a Comment