Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto inawataarifu wanaanchi wote kuwa Kauli
mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mwaka 2014 inasema
”Chochea Mabadiliko Kuleta Usawa wa Kijinsia”. ujumbe huu unasisitiza na
kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuzingatia masuala ya jinsia katika
kuandaa mipango, bajeti na programu za maendeleo katika jamii. Kwa mwaka
2014 maadhimisho yatafanyika katika ngazi ya mkoa.
Wizara itatoa ‘Taarifa kwa Umma’ tarehe0 6/03/2014 ili kutoa ufafanuzi
wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Aidha, Waziri wa Maendeleo
ya Jamii Jinsia na Watoto Mheshimiwa Sophia M. Simba (Mb) atapata fursa
ya kuongea na Waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho na ujumbe wa
kaulimbiu ya Siku ya Wanawake kwa mwaka 2014.
Tunawaomba
Vyombo vya Habari kuendeleza ushirikiano na Serikali na wadau wengine
katika kutangaza, kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu ujumbe maalum
wa kaulimbiu ya Siku ya Wanawake kwa mwaka 2014 pamoja na kuratibu
maadhimisho ili kufikia lengo la kuadhimisha siku hii katika nchi yetu.
Ni
matumaini yangu kuwa kupitia taarifa hii jamii itahabarishwa ipasavyo
na ujumbe maalum wa maadhimisho utasisitizwa kupitia mbinu na matukio
mbalimbali kama yatakavyoibuliwa na kuratibiwa na wadao kataika ngazi
zote.
Erasto T. Ching’oro
Msemaji wa Wizara
Wizara ya Maendeleo ya Jmaii, Jinsia na Watoto
25/02/2014
Post a Comment