Mahakama
kuu mjini Paris nchini Ufaransa inatarajia kuskiliza hii leo kwa mara
ya kwanza kesi ya mauaji ya kimbari yaliotokea nchini Rwanda mwaka 1994
ikiwa ni miaka ishirini tangu mauwaji hayo yatokee.Mtuhumiwa
Pascal Simbikangwa mwenye umri wa miaka 54, na aliyekuwa askari wakati
wa utawala wa Rais Juvenal habyarimana anatarajiwa kufikishwa kizimbani
kujibu mashtaka yanayomkabili ya uhalifu dhidi ya binadamu; tuhuma
ambazo amezitupilia mbali.
Pascal
Simbikangwa alizaliwa mwaka 1959 kijijini Rambura, katika mkoa wa
Gisenyi magharibi mwa Rwanda. Akiwa mshirika wa karibu wa rais Juvénal
Habyarimana, Pascal Simbakangwa alishikilia nyadhifa mbalimbali katika
ikulu ya Rwanda. Mwaka 1982, Pascal Simbikangwa alijiunga na kikosi cha
ulinzi wa rais, baadae katika mwaka wa 1986, Pascal Simbikangwa
alijeruhiwa katika ajali ya gari na kumsababishia madhara fulani. katika
mwaka uliyofuata aliteuliwa kufanya kazi kwenye idara ya ujasusi katika
m akao makuu ya jeshi, kabla ya kuteuliwa mkuu wa idara ya ujasusi ya
Rwanda.
Pascal
Simbikangwa anatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya wapinzani wa utawala
wa rais Juvenal Habyarimana. Anashukiwa pia pia kua mwanaharakati wa
karibu ya utawala wa rais Habyarimana ambao ulijulikana kwa jina la
"Akazu" ikimaanisha 'watu waliyo karibu na familia ya mtawala". Kundi
hili lilikua likiunga mkono kusalia madarakani kwa familia ya Juvenal
Habyarimana, na kua juu na jamii ya wahutu.
Anashukiwa
pia kushiriki kwa kuanzisha kituo cha Radio na Televisheni kiitwacho
(RTLM), kituo ambacho kilichochea chuki dhidi ya watu ktika jamii ya
watutsi. Kwa mujibu wa Mahakama Ya Mauji ya Kimbari ya Rwanda ICTR,
kituo hiki ni moja ya vifaa viliyochochea mauaji ya kimbari yaliyotokea
Rwanda mwaka 1994.
Aidha,
Mashirika ya kiraia yanatarajiwa kuwakilisha upande wa walalamikaji
kwenye kesi hiyo ambayo itarushwa moja kwa moja kwenye vituo vya
televisheni mjini Ufaransa.
Mwenyekiti
wa muungano wa mashirika ya kiraia nchini Ufaransa, Alain Gauthier,
amesema kesi hio ni muhimu kusikilizwa nchini Ufaransa ili raia wa
Ufaransa wajuwe ukweli kwa yale yaliyotokea nchini Rwanda.
“Kesi hii
ya Pascal simbikangwa ni muhimu kwetu kwa sababu kwa mara ya kwanza
itasikilizwa nchini Ufaransa, tukijuwa kuwa mauwaji hayo yamefanyika
nchini Rwanda miaka ishirini iliyopita kwa hiyo ilikuwa jambo muhimu
kusikiliza kesi hiyo, na itakuwa fursa kuwaeleza wafaransa ukweli wa
mambo katika mauwaji hayo, kutoa hukumu kwa mmoja wa watuhumiwa kwa
sababu ni yeye ndiye atakayehukumiwa na sio mauwaji kiujumla”, amesema
Alain Gauthier.
Hayo
yakitarajiwa, Shirikisho la Kimataifa la Haki za Binadamu la FIDH
linaelezea kuridhishwa kwake na kesi hiyo ambayo imesubiriwa kwa siku
nyingi.
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Kimataifa la Haki za Binadamu la FIDH, Patrick Baudoin
ni, amesema kesi hio ni mfano mzuri kwa taifa la Ufaransa, ambalo
limeonekana kwa kipindi kirefu kuwapokea wakimbizi wa Rwanda, hasa
baadhi ya viongoizi waliyohudumu katika utawala wa hayati rais Juvenala
Habyarimana.
“Ni kesi
muhimu sana kwa sababu itasikilizwa nchini Ufaransa, na nchi hii ya
Ufaransa imekuwa moja kati ya mataifa yanayopinga kuwafungulia mashtaka
watuhumiwa wa mauwaji ya kimbari ya Rwanda.
Ufaransa imepokea wakimbizi wengi wa Rwanda na kumekuwepo na hali ya kuwalinda ambayo haikuwawajibisha.
Ufaransa iliunga mkono serikali ya Habyarimana kisisasa na kijeshi, amesema Baudoin.
Wakati
huohuo, uongozi wa waasi wa Rwanda waishio mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo wa FDLR unathibitisha kuweka silaha chini tangu
tarehe 30 mwezi Desemba mwaka uliopita.
Uamuzi
huo unafwatia msimamo wa vikosi vya kimataifa vya kulinda amani nchini
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vya MONUSCO wa kuwasaka na kuwapokonya
silaha waasi hao, ikiwa ni kipaumbele cha vikosi hivyo kwa mwaka 2014 na
tayari harakati za kujianda kwa operesheni hiyo zinaendelea kuripotiwa.
Waasi hao
wameomba viongozi wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu kusimamia mchakato
wa uwekaji silaha chini na kuwasaidia kuwasiliana na serikali ya Kigali
kwa mazungumzo ya amani.
Kaimu mwenyekiti wa waasi wa FDLR, Jenerali Victor Byiringiro, amesema wanasubiri Jumuiya ya Kimataifa kushughulikia madai yao.
“Tutakuwa
wazi, maana yangu ni kwamba kuwaomba viongozi wa Afrika kuingilia kati
ni kwa sababu wanataka Rwanda iwe na amani na nchi hii ya Congo iwe na
amani. Naamini kuwa watatusaidia kutatua tatizo na tutawaonyesha kuwa
tulichokisema ni ukweli na tutawakabidhi silaha zetu”, amesema
Byiringiro.
Watu
yumkini 800,000 kutoka jamii ya watutsi na wahutu wenye msimamo wa
wastani waliuwawa,baada ya kifo cha rais Juvenal Habyarimana mwaka 1994.
Chanzo: kiswahili.rfi.fr


Post a Comment