Mwenyekiti wa
maandalizi ya Kongamano la Viongozi wa Dini mikoa ya Lindi na Mtwara
MohamedSenani akiwakaribisha wajumbe katika kongamano la viongozi hao katika
ukumbi wa VETA mjini Mtwara. Kongamano ambalo viongozi hao walijadiliana juu ya
rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati na Madini Eliakim Maswi akizungumza na viongozi wa dini kutoka mikoa ya
Lindi na Mtwara wakati wa kongamano la viongozi hao lililohusu rasilimali zetu
za gesi asilia, mafuta na madinikwa amani na maendeleo ya Tanzania.
Baadhi ya wajumbe wa
kongamano la viongozi wa dini wakiwasili eneo la Mnazi Bay kujionea shughuli za
namna visima vya gesi vinavyofanya kazi na kuzalisha gesi ambayo ni moja ya
chanzo cha nishati ya umeme kwa maendeleo endelevu ya nchi yetu.
Hiki ni moja ya kisima
cha gesi kilichopo Mnazi Bay eneo la nchi kavu kinachofikisha idadi ya visima
vitatu ambapo kimoja kipo eneo la bahari kuu.
Baadhi ya Viongozi wa Dini
kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara wakitembelea na kujionea eneo ambapo kinajengwa
kiwanda cha kuchakata gesi asili eneo la Madimba ikiwa ni moja ya ratiba
yaokutembelea maeneo mbalimbali wakiwa Mtwara kwenye kongamano lao kujadiliana na kuelimishana juu
ya rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya
Tanzania.
Sheikh Abubakar Zuberi
akitoa mada ya Mtazamo wa Kiteolojia/Kidini juu ya rasilimali za gesi asilia,
mafuta na madini wakati wa kongamano la viongozi hao mjini Mtwara.
Mgeni Rasmi katika
kongamano la viongozi wa dini na Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Tanzania
Dkt. Jacob Chimeledya akifungua kongamano ambapo viongozi hao walijadiliana na
kuelimishana juu ya rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na
maendeleo ya Tanzania.
Baadhi ya viongozi wa
dini wakiwa katika ukumbi wa VETA Mtwara wakisikiliza mada mblimbali
zilizotolewa kataka konganmano la vingozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na
Mtwara.
Baadhi ya viongozi wa
dini wakiwa katika ukumbi wa VETA Mtwara wakisikiliza mada mblimbali
zilizotolewa kataka konganmano la vingozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na
Mtwara. Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO, Mtwara
Post a Comment