Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LIBYA MABINGWA CHAN 2014

 


TIMU ya taifa ya Libya imetwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2014 baada ya kuifunga Ghana kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya bila kufungana Jumamosi Uwanja wa Cape Town.
Ushindi huo ni sawa na Libya kulipa kisasi kwa Ghana baada ya kufungwa kwa penalti 7-6 miaka 32 iliyopita kwenye fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Kipa wa Ghana, Stephen Adams aliokoa penalti mbili za Mohamed Elgadi na Abdelsalam Omar na kufanya mikwaju mitano mitano ya awali imizike kwa sare ya 3-3.

Ahmed El Trbi aliifungia penalti ya sita Libya kabla ya Joshua Tijani kukoa upande wa Ghana na kuamsha shamrashamra za wafalme wa Mediterranean Knights wa Libya.
Katika mchezo uliotangulia kusaka mshindi wa tatu, Nigeria iliifunga Zimbabwe 1-0 na kushinda Medali ya Shaba ya michuano hiyo ya tatu.
Libya inakuwa bingwa wa tatu tangu kuanzishwa CHAN, michuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, wakifuata nyayo za DRC 2009 nchini Ivory Coast na Tunisia 2011 nchini Sudan.

Chanzo:BIN ZUBEIRY
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top